NBAA YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI WA CHUO CBE DAR ES SALAAM - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 1, 2022

NBAA YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI WA CHUO CBE DAR ES SALAAM

 Afisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) kutoka Idara ya Elimu na Mafunzo, Ibrahim Magambo akitoa elimu kwa wanafunzi wa CBE Dar es Salaam ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo kwa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za Sekondari.

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) imeendelea kutoa elimu/mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za Sekondari ikiwa na lengo la kuwajengea ufahamu kuhusu shughuli mbalimbali za Bodi na kukuza taaluma ya uhasibu.

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo Afisa wa NBAA kutoka Idara ya Elimu na Mafunzo, Ibrahim Magambo amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza kufanya kazi za kihasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa cheti cha kitaaluma ili uweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza kufanya kazi nje na ndani ya nchi.

Aliongeza kuwa wanafunzi wa Kozi nyingine ambazo hazihusiani na masomo ya Uhasibu nao wana nafasi ya kufanya mitihani ya Bodi na wataanzia masomo ya ngazi ya kwanza (foundation level) tofauti na wale waliosomea masomo ya Uhasibu  na pia waliomaliza kidato cha nne na sita na wanacheti wanaweza kufanya mitihani ya Bodi

Kutoka kushoto ni Afisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) kutoka Idara ya Elimu na Mafunzo, Ibrahim Magambo akizungumza jambo na kaimu mkuu wa Idara ya Uhasibu CBE Mr Mzungu. 

Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya akifuatilia kwa makini mafunzo hayo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad