MADARAJA MATATU YASOMBWA NA MAJI WILAYANI LUDEWA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 24, 2022

MADARAJA MATATU YASOMBWA NA MAJI WILAYANI LUDEWA

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe


Mvua iliyonyesha siku mbili mfululizo imebomoa madaraja matatu wilayani Ludewa mkoa wa Njombe na kusababisha shughuli za usafirishaji kutoka Ludewa kwenda maeneo mbali mbali kusimama

Madaraja yaliyobomolewa ni Nyapinda njia panda ya kwenda Ibumi,daraja la Muhoro,daraja la chuma la Mhambalasi linalounganisha kata ya Mkomang'ombe na Ibumi pamoja daraja la Ludewa mjini kwenda Ludewa vijijini.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere,amesema mvua hizo zimenyesha usiku febuari 22 na 23 mwaka huu.

Mkuu wa wilaya amewataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiendelea kufanya jitihada za haraka kuweza madaraja ya muda na kuanza kuanza ujenzi wa kujenga madaraja ya kudumu.

Aidha mkuu wa wilaya amesema tayari amefanya mawasiliano na wakala wa barabara Tanroad mkoa wa Njombe ili kuhakikisha hatua za haraka zinachukuliwa ili kunusuru maisha ya watoto wa shule pamoja na wananchi maeneo hayo. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad