HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 21, 2022

TANESCO Manyara watoa Ufafanuzi kwa wananchi kuhusu bei mpya za Umeme

 


Na John Walter-Manyara
Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Manyara, Mhandisi Hamisi Rahisi amesema wamedhamiria kuondoa kero ya kushindwa kuwafungia umeme wateja wake kwa wakati.
Ameeleza kuwa hatma ya wateja wenye namba ya malipo ya bei ya shilingi 27,000,wafike ofisi za TANESCO kwa ajili kupata namba mpya za malipo.
Mhandisi Rahisi amesema hayo Jumatatu Januari 20, 2022 wakati akitoa ufafanuzi kuhusu gharama za kuunganisha huduma ya umeme kwa wananchi wa mkoa wa Manyara, ambapo amesema katika maeneo ya vijijini wataendelea kulipia Sh27, 000 kama kawaida na maeneo ya mjini na miji wataunganishiwa kwa gharama mpya.
Amesema mpango huo wa kuwaungishia umeme wananchi hao ambao walikuwa wamelipia Shilingi 27, 000 utaendelea.
Mhandisi Rahisi amesema Tanesco imeanza kutumia bei mpya za kuunganisha umeme Januari 5 mwaka huu huku ikisema Sh 27,000 itatumika kwenye maeneo ya  vijiji pekee.
Amesema maeneo yatakayolipia gharama halisi za kuunganisha umeme kwa umeme wa njia moja ndani ya umbali wa mita 30 kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni shilingi 320,960, kwa mteja wa njia moja ndani ya umbali wa mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni shilingi 515,618.
Kwa mteja wa njia moja ndani ya umbali wa mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni shilingi 696,670, njia tatu ndani ya umbali wa mita 30 kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni shilingi 912,014.


Ameongeza kuwa kwa mteja wa njia tatu ndani ya umbali wa mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni shilingi 1,639,156.
Kwa upande wa vijijini amesisitiza kuwa kwa njia moja gharama ni shilingi 27,000 na kwamba kikosi maalum kinashughulikia maombi ya zamani yakamilike.
Amesema Chanzo cha bei hizo ni kwa mujibu wa mamlaka ya udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA) ambapo gharama halisi ziliidhinishwa Novemba 25,2020 baada ya kupitia mchakato wa tathmini ya bei kulingana na gharama halisi ya vifaa vya uunganishaji umeme pamoja na uendeshaji.
Kwa upande wake afisa Uhusiano wa TANESCO mkoa wa Manyara Marcia Simfukwe amesema katika maeneo ya Halmashauri ya mji wa Babati yenye kata nane yapo maeneo ambayo yanahesabika vijiji kwa mujibu wa TAMISEMI hivyo yataendelea kuunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi elfu 27,000.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad