HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 29, 2022

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AZIBANA TAASISI ZA FEDHA KUTOA MIKOPO KWA WAKATI KWA WAKULIMA


Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na vyama vya ushirika wa Miwa na Taasisi za Fedha mara baada ya kumalizika kikao. 

Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akichangia  wakati uwasilishaji mada anazozitoa mmoja wa washiriki wa Vyama vya Ushirika wa Miwa.
Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akizungumza katika  Kikao  cha Vyama vya Ushirika wa Miwa na Taasisi za Fedha wakati alipokwenda kupata maoni juu ya kilimo na changamoto zake Kilombelo  mkoani Morogoro.
 
NAIBU Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde amezitaka Taasisi za fedha nchini kutoa mikopo kwa wakati na kwa kuendana na misimu ya kilimo ili mkopo unaotolewa uweze kukidhi dhumuni husika.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 28 Januari, 2022 alipokuwa Kilombero Mkoani Morogoro kushiriki kikao cha viongozi wa vyama vya ushirika wa miwa na Taasisi za fedha.

"Mabenki jitahidini kuendana na msimu au kalenda ya kilimo ili mikopo yenu iweze kutoka kwa wakati na kuwa na tija kwa wakulima wetu. Ninawashauri na kuwaomba muende mkajitafakari na kuja na mfumo wa utoaji mikopo utakaorahisisha huduma, kupunguza muda wa uchakataji na kuongeza tija kwa wakulima.

Lengo la kikao hichi ni kujadiliana kwa uwazi njia rahisi za kumkopesha mkulima wa Tanzania pasipo kuathiri masharti ya kibenki, mfumo wa makubaliano ya utatu (Tripartite Agreement) kati ya Mkulima, Mwenye kiwanda (Mnunuzi) na Benki (Mkopeshaji) umerahisisha sana upatikanaji wa mikopo kwa wakulima tofauti na ule wenye hitaji la dhamana ya mkopo” Alisema Mavunde

Akitoa salamu za wananchi wa Majimbo ya Mikumina Kilombero, kwa niaba ya Mbunge Abubakar Asenga wa Kilombero, Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mh. Dennis Londo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa utatuzi wa changamoto za wakulima wa Bonde la Kilombero ikiwemo kuanza kwa taratibu za awali za ujenzi wa daraja la Bonde la Mto Ruhembe ambalo lilikuwa kikwazo katika usafirishaji wa malighafi ya miwa kwenda katika kiwanda cha Sukari cha Kilombero.

Wakati huo huo viongozi wa vyama vya ushirika wamepongeza kitendo cha Serikali kuja na mfumo wa kupanga maeneo ya uvunaji kwa zone (Zoning) ambao umeondoa kero kubwa iliyokuwa inawakumba wakulima wa Kilombero. Hali hiyo ilipelekea Mhe. Mavunde kuielekeza Bodi ya Sukari Tanzania kwa kushirikiana na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Taifa kuhakikisha maeneo yote yenye wakulima wadogo wa miwa yanapangwa kwa kutumia mfumo huo.

1 comment:

  1. Betway Casino: Online Casino | In-depth Review
    Betway is an online casino from Playtech. They offer a fantastic collection of slots and table games, including 온카지노 사이트 video poker, bingo, blackjack,

    ReplyDelete

Post Bottom Ad