Baadhi ya Wafanyabiashara katika Soko la Bidhaa za Mitumba la Karume Mchikichini, Ilala Dar es salaam wakijaribu kutafuta vitu watakavyoweza kuokoa bila mafanikio kufuatia soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo. Chanzo cha moto huo hadi sasa bado hakijafahamika. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija alifika kwenye eneo la tukio na kuzungumza na wafanyabiashara hao pamoja na viongozi wao, ambapo ameunda tume ya kuchunguza tukio hilo na kutoa siku 14 kwa tume hiyo kukamilisha uchunguzi huo, pia amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha eneo hilo linakuwa kwenye uangalizi maalum na wafanyabiashara hao wameshauriwa kusubiri taarifa ya tume hiyo na kuliana eneo hilo kwa sasa.
Sunday, January 16, 2022

Home
HABARI
MATUKIO MTAANI
MATUKIO KATIKA PICHA: MOTO ULIVYOTEKETEZA SOKO LA KARUME MCHIKICHINI JIJINI DAR ES SALAAM
MATUKIO KATIKA PICHA: MOTO ULIVYOTEKETEZA SOKO LA KARUME MCHIKICHINI JIJINI DAR ES SALAAM
Tags
# HABARI
# MATUKIO MTAANI
MATUKIO MTAANI
Labels:
HABARI,
MATUKIO MTAANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment