HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 26, 2022

JUKWAA LA LADY IN RED LAJA KIVINGINE

Na.Khadija Seif, Michuzi TV


KAMPUNI ya Hugo Domingo lathibitisha kuratibu jukwaa  La Ubunifu wa Mavazi Lady In Red kutimua kivumbi linalotarajiwa kufanyika mapema  Februari 12 katika ukumbi wa Serena jijini Dar es salaam.

Akizungumza na kuhusiana na Maandalizi ya awali ya jukwaa hilo, Mratibu Marry Fernandez amesema kuwa onesho la Mwaka huu litakuwa tofauti na Miaka mingine.

"Kutokana na mwamko wa watanzania wengi kupenda kuvaa Mavazi ya wabunifu wa ndani hivyo jukwaa hili ni fursa Kwa wabunifu kuchangamia Soko Kwa kuandaa Mavazi Bora."

Hata hivyo Mbunifu wa Mavazi Didas Kantona ameeleza Kwa namna ya onesho la mwaka huu lilivojumuisha wabunifu watatu ambao ni walemavu wa Macho.

"Jumla yha wabunifu 17 watashiriki katika onesho  Hilo na miongoni mwao wabunifu watatu ni walemavu wa macho.

Aidha Kantona ameeleza lengo la jukwaa Hilo no kuhakikisha sekta ya ubunifu wa Mavazi inachangia fedha nyingi katika Pato la taifa,kuwa na viwanda vingi vya ubunifu wa Mavazi vinavyoweza kuzalisha kwa wingi na kuuza nje ya nchi.

Pia amewaomba wadau wa jukwaa la ubunifu wa Mavazi kujitokeza Kwa wingi  katika onesho hili Ili kuwatia Moyo wabunifu hususani walemavu wa Macho.

  

Mratibu wa jukwaa la ubunifu wa Mavazi Lady in Red Marry Fernandez akisikiliza Kwa makini swali kutoka Kwa Waandishi Wahabari akiwa pamoja na Mbunifu wa Mavazi  Didas Kantona pamoja na Muwakilishi kutoka Kwa Hugo Domingo Harith Juma

    

Mbunifu wa Mavazi Lady in Red Kwa miaka iliyopita Didas Kantona akitolea ufafanuzi  swala la wabunifu watakaoshiriki katika Onyesho hilo

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad