IGP SIRRO AWAVALISHA NISHANI MAOFISA, WAKAGUZI NA ASKARI 123 DODOMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 22, 2022

IGP SIRRO AWAVALISHA NISHANI MAOFISA, WAKAGUZI NA ASKARI 123 DODOMA

 MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amewavalisha nishani maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 123 waliotunukiwa nishani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Samia Suluhu Hassan.

Akisoma taarifa ya kuvisha nishani hizo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mihayo Msikhela, amesema kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa mamlaka aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ametunuku nishani ya miaka 60 ya uhuru, nishani ya utumishi uliotukuka na nishani ya utumishi mrefu na tabia njema.Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, akiwavalisha nishani maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 123 jijini Dodoma Januari 22, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad