WLAC WATOA ELIMU YA KUPINGA UNYANYASAJI WA KIJINSIA, WANAFUNZI WAASWA KUTOA TAARIFA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 1, 2021

WLAC WATOA ELIMU YA KUPINGA UNYANYASAJI WA KIJINSIA, WANAFUNZI WAASWA KUTOA TAARIFA

Afisa Sayanskimu Temeke, Rosemary Mmasa akizungumza wakati wa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Kingugi iliopo Mbagala jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2021.
Mratibu wa Mradi wa ulinzi na Usalama kwa watoto kutoka kituo cha Msaada wa Kisheria kwa watoto na wanawake, Wakili Abia Richard akizungumza wakati wa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya msingi Kingugi Mbagala jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2021.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
KATIKA kukabiliana na Vitendo vya ukatili wa Kijindia kwa watoto, Kituo cha msaada wa Kisheria kwa Watoto na wanawake (WLAC) wametoa elimu kwa wa wanafunzi, walimu na wazazi wa Shule ya Msingi Kingugi iliyopo Mbagala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo leo Desemba Mosi, 2021 Mwakilishi wa Afisa Elimu Wilaya ya Temeke, Afisa Sayansikimu Temeke, Rosemary Mmasa amewaasa wanafunzi kuwa makini, kutoa taarifa za matukio yote ya ukatili wanayofanyiwa nyumbani, barabara na shuleni na katika jamii kwa ujumla ili yaweze kukemewa vikali.

"Watoto semeni, ondoeni ukimya  semeni sasa ukatili ni basi." Amesisitiza Rosemary

Amesema kuwa watoto wanatakiwa kuwa wakweli pale ambapo wanaulizwa juu ya changamoto zinazowakabili hata hivyo walimu wameaswa kuwasikiliza watoto pale ambapo watoto wanatoa taarifa juu ya ukatili wa wanaofanyiwa ili waweze kutatua wakishirikiana na ustawi wa jamii pamoja na dawati la jinsia katika vituo vya polisi nchini.

Amesema kuwa mtoto ili aweze kujifunza vizuri lazima asiwe na hofu ya kitu chochote, wazazi nao wameaswa kuwapa watoto haki za msingi ili watoto waweze kufikia malengo yao ya Kielimu.

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo leo,  Mratibu wa Mradi wa ulinzi na Usalama kwa watoto kutoka kituo cha Msaada wa Kisheria kwa watoto na wanawake, Wakili Abia Richard amesema kuwa siku 16 za kupinga ukatili jinsia kwa mtoto zitasaidia kuongeza ulinzi kwa mtoto na kutoa taarifa juu ya masuala ya ukatili kwa mtoto akiwa nyumbani na shuleni.

Amesema kuwa Wameshatoa elimu kwa shule za msingi 10 za jijini Dar es Salaam pamoja na kufungua Clabu za kupinga ukatili kwa mtoto ili kuhakikisha wanaimarisha ulinzi kwa watoto dhidi ya unyanyasaji wanaofanyiana wao kwa wao, we anaofanyiwa na wazazi nyumbani.

Licha ya kutoa elimu kwa walimu na watoto lakini WLAC wameshawafikia maafisa ustawi wa jamii 60, Maafisa dawati ya jinsia kwa watoto katika vituo vya Polisi zaidi 80 vilivyopo jijini Dar es Salaam.

Kauli mbiu ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto mwaka huu ni "Ewe mwananchi komesha vitendo vya ukatili sasa."

Akitoa ombi kwa wadau wa maendeleo ya mtoto, Afisa Elimu wa kata ya Kibulugwa iliyopo Mbagala, Julius Mbwaga amewaomba WLAC kutoa mafunzo hayo kwenye kamati za shule kwani kamati hizo zinamkusanyiko wa watu  mbalimbali.

Amesema wadau hao wanatoka katika serikali za mtaa na baadhi ya wazazi wa wanafunzi hivyo wanaweza kwenye kutoa elimu katika ngazi za mitaa yao na wazazi watatoa elimu kwa watoto wao na wazazi wengine.

Upande wa Mwakilishi wa Dawati la jinsia na watoto kutoka kituo cha Polisi Mbagala, Benard Msuya amesema kuwa katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wameweza kukemea vikali juu ya masuala yote yanayonyang'anya baadhi ya haki za bianadamu pamoja na kutoa elimu juu ya  katili wa watoto majumbani na shuleni.

Amesema wameweza kutoa elimu ya haki za watoto ya mwaka 2009 na wameweza kuwaelimisha watoto kujua haki zao za msingi.

Kwa upande wa Mkuu wa shule ya Msingi Kingugi, Merikiori Kamagi ametoa wito kwa WLAC kuongeza wigo katika kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi ili kukomesha unyanyasaji wa kijinsia unaofanyika kati ya mwanafunzi na mwafunzi, kati mwalimu na mwanafunzi na ukatili unaofanyika majumbani ili watoto waweze kutoa taarifa.
Afisa Elimu Kata ya Kibulugwa Julius Mbwaga akizungumza wakati wa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Kingugi iliopo Mbagala jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2021.
Mkuu wa shule ya Msingi Kingugi, Merikiori Kamagi akizungumza wakati wa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Kingugi iliopo Mbagala jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2021.
Mwakilishi wa Dawati la jinsia na watoto kutoka kituo cha Polisi Mbagala, Benard Msuya akizungumza wakati wa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Kingugi iliopo Mbagala jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2021.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kingugi wakionesha michoro waliyoichora kuonesha ukatili wanaofanyiwa watoto na wanafunzi katika jamii zao na majumbani wakati wa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Kingugi iliopo Mbagala jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2021.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kingugi wakiwa katika maadhimisho siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Kingugi iliopo Mbagala jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2021.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kingugi wakiimba ngonjera walizoziandaa wakati wa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Kingugi iliopo Mbagala jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2021.
Mwakilishi wa kamati ya shule ya Msingi Kingugi akitoa neno la shukurani  wa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi hiyo iliopo Mbagala jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2021.
Picha ya pamoja.
Wanafunzi wakitoa burudani kwa wageni waalikwa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad