HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 4, 2021

Wanataaluma ARU wapigia debe umuhimu wa mipango miji


Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo la wanataaluma wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), akichangia mada wakati wa kongamano hilo lililofanyika chuoni hapo siku ya Ijumaa ambapo mada kuu ilikuwa kuelekea kwenye kupatikana ardhi na makazi nafuu kwa kaya zenye kipato cha chini miaka 60 baada ya Uhuru.Na 

Mwandishi Wetu
WANATAALUMA wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wameishauri serikali kulipa kipaumbele suala la mipango miji kwa kuhakikisha maeneo mengi yanapimwa na kuwekewa huduma muhimu ili wananchi wanapofika wasijenge holela.

Ushauri huo umetolewa Desemba 3, 2021 na Mwenyekiti wa kongamano la tisa la wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Haruna Masebu, wakati wakijadili masuala ya mipango miji, ardhi na makazi nafuu.

Mada kuu kwenye kongamano hilo la wanataaluma wahitimu wa chuo hicho ilikuwa kuelekea kwenye kupatikana kwa ardhi na makazi nafuu kwenye kaya zenye kipato cha chini nchini miaka 60 baada ya Uhuru.

Masebu amesema wameamua kuzungumzia masuala ya makazi nafuu kuangalia namna nchi ambavyo imesaidia wananchi wake tangu uhuru kupata makazi nafuu kwa kuwa makazi ni jambo la msingi kwa binadamu.

“Tumeona ni vizuri kuangalia tulipotoka tulipo na tunapoelekea kwenye suala la makazi ila tumeona changamoto kubwa ya watu kuishi kwenye maeneo ambayo hayajapimwa wanaishi sehemu hazijapangwa hivyo wanakosa huduma muhimu,” alisema

Amesema kuna umuhimu kwa serikali kuweka mipango kuhakikisha wananchi wanaishi na kujenga kwenye maeneo yaliyopangwa kwa kuweka miundombinu na mahitaji yote muhimu.

Amesema bado kuna changamoto ya kupata fedha za kujenga makazi hivyo wanatumia muda mrefu kujenga nyumba hivyo wasomi wamejadili namna ya kuwezesha wananchi kujenga kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi.

Amesema miongoni mwa majukumu yanayowakabili wanakongamano hao niq kujenga taasisi imara yenye heshima ni kuhakikisha hosteli za chuo hicho zinakuwa na taa za barabarani na kujenga jingo kubwa litakalokuwa na shughuli mbalimbali.

“Kongamano hili linapaswa kushirikiana na ARU na washirika wengine katika kutimiza majukumu yake na mafanikio yetu mengi yatategemea namna tunavyoshirikiiana na wengine hivyo natoa wito kwa baraza la wahitimu kufanyakazi kwa bidii, kuweka mikakati kabambe na kuwa na maono ya muda mrefu kuhakikisha shughuli zote zinafanyika kwa haraka na kwa wakati,” alisema
Profesa Joseph Lusegga ambaye ni mbobezi kwenye masuala ya ardhi akizungumzaa kwenye kongaamano la wanataaluma waliowahi kusoma kwenye Chuo Kikuu Ardhi lililofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam ambapo mada kuu ilikuwa kuelekea kwenye kupatikana ardhi na makazi nafuu kwa kaya zenye kipato cha chini miaka 60 baada ya Uhuru.
Washiriki wa kongamano la wanataaluma waliowahi kusoma  Chuo Kikuu Ardhi (ARU), wakifuatilia kwa karibu mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kongamano lililofanyika chuoni hapo siku ya Ijumaa. Kushoto kabisa ni Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Haruna Masebu.
Washiriki wa Kongamano la wanataaluma wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo lililofanyika chuoni hapo jana jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad