Serikali yatoa taarifa ya abiria aliyepatikana na anuwai mpya ya UVIKO-19 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 6, 2021

Serikali yatoa taarifa ya abiria aliyepatikana na anuwai mpya ya UVIKO-19

 


*Yataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa ,ukaguzi kuanza katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma kwa wananchi.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Serikali imetoa ufafanuzi wa abiria aliyeripotiwa kuwa na anuwai mpya ya UVIKO -19 (OMICRON) nchini India na kudaiwa ametokea Tanzania na wito umetolewa wa kuendelea kuchukua tahadhari za kinga za ugonjwa huo.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Abel Makubi amesema kuwa Wizara kupitia Maabara Kuu ya Taifa, imekuwa ikisimamia upimaji wa ugonjwa wa UVIKO-19 nchini ikiwa ni pamoja na kuangalia anuwai mpya zinazoshabibishwa na mabadiriko ya mara kwa mara ya kirusi cha UVIKO-19.

Profesa Makubi amesema hivi karibuni kumetokea unuwai mpya ijulikanayo kama Omicron (B.1.1.529) iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza Afrika ya Kusini na Botswana.

Amesema taarifa ya Desemba 5,2021 iliyoripotiwa na vyombo vya habari vya India na kuenea katika mitandao ya kijamii na kueleza kuwa India waamegundua abiria mmoja anayerudi nyumbani (India) mwenye anuwai mpya Omicron ambaye ametokea Tanzania hata hivyo haijajulikana kama abilia huyu alitokea Tanzania moja kwa moja au alipita Tanzania kuelekea India na haijulikania alipita wapi kabla ya kufika India.

Katibu Mkuu huyo amesema kutokana na taarifa hizo, Wizara ya afya imeanza kufatilia kupitia vyombo vyetu vya ndani na pia kwa kushirikiana ubalozi wa Tanzania nchini India ili kubaini ukweli wa jambo hili na baadae kuchukua hatua stahili.

"Nipende kuwasihi Wanachi kutokuwa na hofu kutokana na habari hii, bali tuendelee kuwa watulivu na kutekeleza shughuli za maendeleo huku tukichukua taadhali zote. Ikiwa pamoja na Kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, kuvaa barakoa na kujiepusha na misongamano isiyokuwa ya lazima na kufuata miongozo mbali mbali inayotolewa na Wizara kupambana na UVIKO-19"amesema Profesa Makubi

Hata hivyo amesema Wizara imeendelea kuchukua hatua zaidi za kuepusha nchi yetu isiingie kwenye mlipuko wa nne kwa kuendelea na upimaji kwenye mipaka na viwanja vya ndege. Kama taratibu zilivyo nchi zingine watu wote wanaosafiri kwenda nje ya nchi kwa shughuli mbali mbali hupimwa UVIKO-19. 

Wasafiri wanaogundulika hawana maambukizi ya UVIKO-19 kwa kutumia kipimo cha RT-PCR hupewa cheti kuwaruhusu kusafiri na wasafiri wanaogudulika kuwa na maambukizi huunganishwa na Daktari/Hopsitlai ili waanze matibabu, kuwa katika uangalizi maalumu na kufatiliwa contacts wake.

Maabara ya Taifa pia imekuwa ikichunguza mabadiriko ya kirusi (Gene sequencing) kuangalia uwepo wa anuwahi mbali mbali zinazotokana na mabadiriko ya UVIKO-19 ikiwemo anuwai mpya ya Omicron.

"Tunaomba kuwatoa wasi wasi watanzania wote kuwa mpaka sasa hatujabaini anuwahi mpya ya UVIKO-19 (Omicron) ,tunao uwezo wa kubaini anuawahi hii mpya ya Omicron na tunaendelea kuzifuatitilia sampuli zote tukibaini uwepo wa anuwahi mpya tutatoa taarifa. 

Aidha mpaka sasa uchunguzi zaidi ya wanasayamsi duniani unaendelea kujua anuai hii ya Omicron ina madhara ya kiasi gani kwa mtu anapoambukizwa. Mpaka sasa taarifa kutoka mataifa yaliyobaini wananchi weny virusi hivi, wamekuwa na dalili za kiasi na nyepesi bila kuingia mahututi"amesma

Amesema Viogozi wote wa Mikoa na Wilaya kuweka na kukagua miundo mbinu hasa hasa sabuni na maji ya kunawa mikono sehemu za mikusanyiko ili tuwekeze katika kujikinga na UVIKO-19 bila kusubiri athari kubwa ikiwemo kupoteza maisha baada ya kupata maambukizi.

Wizara inawahimiza wananchi kujitokeza kuchanja ili kujikinga na UVIKO-19 na kuanzia tarehe 07/-10/12/2021 tutakuwa na Kampeni Maalumu za elimu za kuhamasisha wananchi wengi zaidi wajitokeze kuchanja katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa nchi yetu. Kampeni hizo zitafanyika katika ngazi za Mitaa, Masoko, Viwanja vya mipira, Stand za bus/daladala, ,Vyuo na kweye taasisI mbalimbali.

Hata hivyo alibainisha viongozi wote katika Mikoa, Wilaya,Mitaa na vijiji, tusimamie zoezi hili kwa ufanisi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Profesa Abel Makubi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taarifa ya abiria aliyeripotiwa kuwa na Anuwai mpya ya UVIKO-19 (OMICRON) akitokea Tanzania ,jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto Profesa Abel Makubi akizungumza kwenye maabara ya Taifa namna wanavyochukua Sampuli na kuzima katika maabara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad