Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
 Mulamula akizungumza baada ya kumalzika kwa mkutano wa nane wa Mawaziri
 wa Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC
Na Mwandishi wetu, Dakar
Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
 Mulamula (Mb) amesema mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Ushirikiano kati 
ya China na Afrika (FOCAC) kimefanyika kwa mafanikio makubwa.
Balozi
 Mulamula ametoa kauli hiyo jijini Dakr nchini Senegal baada ya 
kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika Novemba 29 na 30 2021 nchini 
humo.
Amesema
 kikao hicho kimekuwa cha mafanikio kwani kimepitisha maazimio makubwa 
na mpango kazi ambao umejikita katika kutekeleza maeneo ya kimkakati 
ambayo yakisimamiwa kikamilifu yatazinufaisha nchi za Afrika .
Balozi
 Mulamula amesema kauli ya China ya kuzihakikishia nchi za Afrika kuwa 
itasaidia kuanzisha viwanda vya kuzalisha chanjo za COVID 19 pamoja na 
dawa nyingine ni ya kujivunia na ya kupongezwa.
"Tanzania
 imefurahishwa na ahadi hiyo kwani jambo hilo litazifanya nchi za Afrika
 kuwa na uwezo wa kuzalisha chanjo na dawa nyingine kwa ajili ya 
kuwalinda watu wake na kuacha kutegemea msaada., kauli ya Rais Jinping 
ni ya kujivunia na ya lupongezwa,"amesema Balozi Mulamula.
Amesema
 kikao kimekuwa na mafanikio zaidi kwani mbali na kuangalia maeneo ya 
siku zote ya kuendeleza miundombinu na viwanda, kwa mara ya kwanza 
umeangalia jinsi ya kusaidia na kuendeleza wafanyabiashara wadogo na wa 
kati.
Amesema
 uamuzi wa China kwa kutoa kipaumbele katika eneo la kujenga viwanda vya
 kuzalisha dawa na chanjo na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wa 
kati ni wa kupongezwa mno kwani mambo hayo ndiyo ambayo Tanzania 
ilitilia mkazo katika taarifa yake na kuongeza kuwa wamefarijika kwamba 
Rais Jinping ameahidi kusaidia katika eneo hilo.
“Jambo
 hili ni zuri na kubwa sana, ni miongoni mwa maeneo ambayo Tanzania 
iliyasemea, eneo hilo ndiko watu wengi walikopata ajira hasa akina mama 
na vijana tunaishukuru na kuipongeza China  kwa kutoa kipaumbeele katika
 eneo hilo”, alisema Mhe. Waziri.
Amesema
 kikao hicho pia kimeangalia maeneo ya kujengea uwezo wananchi wa Afrika
 katika eneo la ufadhili wa masomo ambalo kwa wakati huu limekwama 
kutokana na mlipuko wa virusi vya Covid 19 lakini wameahidi kuendelea 
nalo pale hali itakapotengemaa.
Ameongeza
 kuwa kikao pia kimeangalia suala la kuendeleza kilimo ili kuwa na 
kilimo cha kisasa na kuendeleza miundombinu ya kidijitali hasa nyakati 
hizi ambazo ni lazima kujiunganisha kidigitali ili kujikwamua  kiuchumi.
Amesema
 China imesisitiza na kuweka mkazo katika eneo la kundeleza kilimo ili 
kuziwezesha nchi za Afrika kujikwamua na umasikini na wameahidi kutoa 
fedha na kuleta wataalamu kwa ajili ya kuendeleza kilimo.
Mkutano
 huo wa siku mbili ulijumuisha viongozi na wawakilishi kutoka Bara la 
Afrika na China uliangalia jinsi China ilivyotekeleza hatua za 
ushirikiano kwa kipindi cha miaka mitatu cha 2018-2021 kwenye  maeneo ya
 miradi ya kimkakati na ukuzaji wa wigo  wa biashara kati ya China na 
mataifa ya Afrika.

No comments:
Post a Comment