CHUO KIKUU MZUMBE WAOMBA WAWEKEZAJI KWENDA KUWEKEZA, MAHAFALI YA 20 YAFANA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 8, 2021

CHUO KIKUU MZUMBE WAOMBA WAWEKEZAJI KWENDA KUWEKEZA, MAHAFALI YA 20 YAFANA

Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam wakishanguilia mara baada ya kutunukiwa Sahada za umahiri katika Mahafali ya 20 ya Ndaki ya Dar es Salaam leo Desemba 8, 2021. Mahafali hayo yamefanyika katika Viwanja vya Kituo cha Dar es Salaam.


Na Avila Kakingo, Globu ya jamii
WAHITIMU wa Mahafali ya 20 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar Es Salaam wameaswa kwenda kufanya kazi kwaajili ya watu kama kauli mbiu ya chuo hicho inavyosema.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka amesema hayo wakati wakati wa Mahafali ya 20 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 8, 2021 katika uwanja wa kituo cha Tegeta ambako hutolewa shahada ya kwanza.

Amesema kuwa wahitimu wa Chuo hicho Ndaki ya Dar es Salaam wameiva, waajili waliokuwa na shaka ya kuwapa vyeo wanaweza kuwapa vyeo hivyo kwani wanawajibika vizuri.

Amesema anatamani wahitimu hao wakafanye kazi kwaajili ya watu ambapo taifa limewekeza kwao, kwakuweza mazingira hayo ambayo kila mtanzania amewekeza kwa namna yake.

"Mkiondoka kwa kujua hilo mnaweza kuwahidumia watanzania vizuri bila kuchukua Rushwa, bila kuwa na dhuruma yeyote na kutokuwa na ufisadi wowote." Prof. Kusiluka amewaasa Wahitimu

Licha ya hayo amewaalika wahitimu hao Kusoma PHD katika Chuo hicho kwani wanampango wa kutengeneza kituo cha PHD. (PHD Centre) kwa kubadilisha mazingira katika Kampasi Kuu ya Morogoro.

Hata hivyo amewaalika wawekezaji kuwekeza katika chuo hicho Ndaki ya Dar Es Salaam katika kituo cha Tegeta kuwekeza katika ujenzi wa Hosteli pamoja na maduka.

"Tunawakaribisha sana wale ambao walikuwa hawajaona uwekezaji hapa, tunayo sera ya uwekezaji ya chuo Kikuu Mzumbe inayoongoza mambo ya uwekezaji yanavyofanyika katika eneo hili." Amesema Profesa Kusiluka

Akizungumza kuhusu Mipaka ya Chuo hicho, Profesa Kusiluka amewaomba wananchi wanaozunguka mipaka ya kituo cha Tegeta kutokuingia kwenye mipaka ya eneo la chuo hicho.

"Tunatamani sana kuishi vizuri na majirani zetu, tunaomba wasogee lakini wasiingie kwenye mipaka yetu." Amesisitiza Prof. Kusiluka.

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kualika wawekezaji kuweza nchini ili kwani itaongeza wahitumu wa nchini kuajiliwa.

Katika Mahafali hayo uongozi wa Chuo kikuu umewatambua Wanataaluma 10 waliofanya vizuri katika kuchapisha machapisho ya tafiti mbalimbali pamoja na waliofanya vizuri katika masomo yao kwa kuwapa vyeti na zawadi.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe ambaye pia ni Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Mohamed Ali Shein, akisaini kitabu cha wageni alipowasili Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kituo cha Tegeta kwa ajili ya Mahafali ya 20.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akitoa taarifa ya chuo kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe ambaye pia ni Rais mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein akiwa katika picha ya pamoja na Baraza la chuo.
Maandamano ya kitaaluma katika mahafali ya 20 ya chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo Desema 8, 2021 katika Viwanja vya  kituoa cha TegetaMakamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka akizungumza katika Mahafali ya 20 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam katika viwanja vya Kituo cha Tegeta le Desemba 8, 2021.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad