Tanzania Timu ya Kwanza Kufuzu Canaf Afrika Kwenda Robo Fainali - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 30, 2021

Tanzania Timu ya Kwanza Kufuzu Canaf Afrika Kwenda Robo Fainali

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka kwa Wenye Ulemavu (Tembo Warriors), imeipa hadhi nchi kwa kuwa Taifa la kwanza Afrika, kufuzu kwenda Robo Fainali za Mashindano ya Soka kwa Walemavu Afrika (Canaf), ambayo Tanzania ni mwenyeji.

Tanzania imepata nafasi hiyo baada ya leo kuifunga timu ngumu ya Taifa ya Sierra Leone bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

“Sasa tuna mechi moja mbele kabla ya kupata tiketi mbili muhimu; moja ni kuingia nusu fainali lakini tukishinda mechi hiyo moja pia tutakuwa tumefuzu moja kwa moja kwenda Kombe la Dunia litakalofanyika mwakani mjini Instanbul, Uturuki,” alisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na wachezaji hao baada ya mechi.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad