Wataalam
wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wapo mkoani Iringa katika zoezi la
kusajili Skimu za Umwagiliaji pamoja na kutoa elimu ya Ada na Tozo kwa
viongozi wa vyama vya wamwagiliaji.
Akizungumza
na Viongozi wa Skimu ya Mangalali iliyopo Wilaya ya Iringa Vijijini,
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mazingira Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw,
Fumba Malima amewaeleza viongozi hao kuwa, suala la kulipa Ada na Tozo
za Umwagiliaji lipo kisheria na sio hiari na kuwataka viongozi wa Skimu
ya Mangalali kusimamia kwa weledi zoezi la ukusanyaji Ada na Tozo za
Umwagiliaji ili kuharakisha maendeleo ya sekta ya Umwagiliaji nchini.
“Fedha
hizo ndizo zitakazotumika kukarabati Miuondombinu ya Umwagiliaji
iliyoharibika katika Skimu zenu, pamoja na kujenga Skimu mpya kufikia
Hekta Milioni Moja na Laki mbili mwaka 2025, kama ilani ya chama Tawala
inavyoelekeza”.
Kwaupande
wake Afisa Kilimo kutoka Tume Bi,Restuta Mushi, ametumia fursa hiyo
kuwaelimisha viongozi hao, njia inayotumika kulipia Ada na Tozo za
Umwagiliaji ambapo mhusika anapaswa kufanya malipo kupitia namba maalum
ya Malipo itakayotolewa na idara ya uhasibu ya Tume, lakini pia amewapa
fomu maalum itakayorahisisha zoezi la kuhamisha fedha za Ada na Tozo
kwenda akaunti ya Mfuko wa Umwagiliaji mara baada ya chama hicho kuingia
makubaliano na benki wanayohifadhia fedha zao.
Mtaalam
wa masuala ya Umwagiliaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa
Bw,Bonaventure Mkude amesema makusanyo ya Tozo katika Skimu hiyo ni
yakusuasua kwasababu hapo nyuma hakukuwa na matumizi ya sheria ya
Umwagiliaji, hivyo kulipa faini ya Tsh, milioni moja au kwenda jela
mwaka mmoja, ama vyote kwa pamoja, itasaidia zoezi la ukusanyaji wa Ada
na Tozo za Umwagiliaji kufanyika kwa wakati na zoezi hilo kuwa endelevu
kwakuwa ni takwa la kisheria.
Mwandisi
wa Umwagiliaji wa Tume Mkoa wa Iringa, Bw, Onesmo Kahoggo amewashauri
viongozi hao wa Skimu ya Mangalali kumshirikisha katika vikao vyao na
wakulima ili aweze kufafanua kwa karibu zaidi umuhimu wa kulipa Ada na
Tozo za Umwagiliaji sanjari na faida watakazopata wakulima wa Skimu hiyo
kutokana na michango yao kila msimu wa mavuno.
Viongozi
wa Skimu hiyo wameahidi kujisajili Tume ya Taifa ya Umwagiliaji pamoja
na kulipa Ada na Tozo kwa wakati kwa mujibu wa sheria.
Skimu ya Mangalali ina jumla ya wanufaika 250.
Kaimu
Mkuu wa kitengo cha Mazingira Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (Wa pili
kushoto ) Bw, Fumba Malima akitoa elimu kwa Viongozi wa chama cha
Wamwagiliaji Skimu ya Mangalali kuhusu sheria ya Umwagiliaji na takwa la
kisheria la kulipa Ada na Tozo. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Skimu ya
Mangalali Bw, Piero Ngahega, akisikiliza kwa makani.
Kushoto
kwa Bw, Fumba Malima ni Bi, Restuta Mushi afisa kilimo Tume na
anayefuatia ni Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Iringa Bw, Onesmo
Kahoggo.
Bw,
Bonaventure Mkude, Mtaalam wa Masuala ya Umwagiliaji Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa akichangia mawazo yake kuboresha mikakati ya ukusanyaji
wa Ada na Tozo za Umwagiliaji.
Picha za kilimo cha Mahindi, Nyanya na Mbogamboga katika Skimu ya Mangalali Iringa Vijijini.
No comments:
Post a Comment