HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 31, 2021

Watumiaji wa Vodacom M-Pesa Wagawiwa Faida ya Shilingi 5.1Bilioni

Vodacom Tanzania Plc imeanza kutoa mgao wa Shilingi 5.1 bilioni kwa watumiaji wake zaidi ya 10 milioni, ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana kwenye akaunti za M-Pesa. Malipo haya yanategemewa kukamilika tarehe 31 Oktoba, ambapo wateja wote watakuwa wameshapokea mgao wao.

Akifafanua kuhusu gawio hilo la M-Pesa, Mkurugenzi wa M-Pesa Epimack Mbeteni, alisema, “tuna furaha kubwa sana kuona kuwa pamoja na changamoto za mazingira ya biashara ambayo wateja wetu wamekuwa wakikabiliana nayo, huduma ya M-Pesa inaendelea kuwa msingi wa shughuli za kibiashara hapa nchini. 

Tuko katika mchakato wa kugawa Shilingi bilioni 5.1 kwa wateja wetu ambao wamekuwa wakitumia mfumo wetu kwa kipindi hiki, na malipo yanaingia moja kwa moja katika akaunti zao za M-Pesa.”

Faida italipwa kwa wateja, mawakala, wakala mkuu na wadau wengine wa kibiashara wa M-Pesa kulingana na matumizi yao ya huduma za M-Pesa. Gawio linategemea kiasi cha matumizi ya huduma katika kipindi hicho cha robo ya pili ya mwaka.

Shughuli hizo ni pamoja na kuhamisha pesa, kulipa bili, manunuzi ya muda wa maongezi na mengine.
Wateja wanaweza kutuma neno “KIASI” kwenda namba 15300 ili kuona kiasi cha gawio watakalopokea. 

Mara baada ya kupokea mgao, wateja wa M-Pesa wanaweza kutumia gawio hilo kwa njia ya kutoa pesa taslimu, kununua vifurushi vya maongezi na data au kutumia kulipia bili au manunuzi ya bidhaa.

Bw. Mbeteni alimalizia kwa kusema, “Mfumo huu wa kipekee umekuwa na nafasi kubwa katika kujenga hali ya ushirikishwaji na upatikanaji wa huduma za kifedha nchini. Wanawake na vijana wameona unafuu na urahisi wa kutumia M-Pesa na wanatumia huduma nyingi ili kuboresha maisha yao. 

Pia mfumo umekuwa rasilmali muhimu katika kuwezesha biashara ndogondogo na kupambana na changamoto zilizosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19. 

Kwetu Vodacom Tanzania, dhamira yetu ni kuhakikisha kuwa mfumo huu unaendelea kuwa mfumo unaoendana zaidi na mahitaji ya wateja.”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad