Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imepokea shilingi bilioni 1,720,000,0000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari 23 na ujenzi wa madarasa katika shule shikizi za msingi 3.
Akizungumza kwenye kikao kilichoitishwa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius kenneth Ningu katika ukumbi wa Halmashauri Afisa mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Amos Kanige alisema kuwa Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi 1,720,000,000 kutoka serikali kuu Kwa ajili ya kujenga madarasa kwenye shule za sekondari 23 na kujenga madarasa katika shule shikizi za msingi 3.
Afisa Elimu shule za Msingi bwana Protas Komba alisema amepokea kiasi cha shilingi milioni120 kwa ajili ya shule shikizi 3 zilizopata fedha hizo ni Mhekela,Nandengele na Ujamaa ikiwa kila shule shikiki imepewa shilingi milioni 40.
Naye afisa elimu Sekondari Roza Nabahani kwa upande wake alidai amepokea kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kutoka serikali kuu kwa ajili ya kujenga madarasa katika shule za sekondari 23 za Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Chiriku Hamisi Chilumba katika kikao hicho alimhakikishia mkuu wa wilaya kuwa shule zote zilizopata fedha kwa ajili ya kujenga madarasa yatasimamiwa kwa karibu na ofisi yake ili kuhakikisha adhima ya serikali ya kujenga madarasa iweze kutimia.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo kwa upande wake alidai hayupo tayari kuona ujenzi wa madarasa katika wilaya yake kujengwa kwa kiwango kisichoridhisha na kuwataka wasimamizi wa miradi hiyo kusimamia ujenzi kwa kiwango kinachotakiwa na serikali.
“ Ole kwenye hii awamu atakayebainika kushindwa kusimamia mradi katika idara yake ipasavyo na kusababisha malalamiko yasiyo ya lazima kwa jamii katika eneo linalotekeleza mradi huo “ alisema mkuu wa wilaya huyo.
Kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa idara na vitengo,watendaji wa kata ,makatibu tarafa,walimu wakuu na wakuu wa shule wenye miradi na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ambapo kwa pamoja wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika kutekeleza miradi ya ujenzi
No comments:
Post a Comment