HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 4, 2021

MAJALIWA: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUTEKELEZA DHANA YA UCHUMI JUMUISHI KWA VITENDO

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kutekeleza dhana ya uchumi jumuishi kwa vitendo kwa kuweka vipaumbele vitakavyowawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 4, 2021) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, jijini Dodoma. Amesema kuwa vipaumbele katika mipango ya Serikali vimekuwa katika utekelezaji wa shughuli za kiuchumi zinazowajumuisha moja kwa moja wananchi.

Waziri Mkuu ametaja baadhi ya vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na uimarishaji wa huduma za afya, hifadhi ya jamii, maji, umeme na utekelezaji wa mpango wa elimumsingi bila ada “Mtanzania mwenye afya, aliyeelimika na miundombinu wezeshi ni chachu kwa ukuaji uchumi wa nchi yetu.”

Amesema uwezeshaji wa uchumi jumuishi ni msingi wa kuhakikisha kunakuwa na ustawi endelevu kwa watu wote, ambapo Serikali imeandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 ambayo pamoja na mambo mengine imeainisha mazingira wezeshi yatakayowezesha nchi kunufaika kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 pia imelenga kuhakikisha kunakuwa na viwango vya juu vya maisha, amani na umoja, utawala bora na uchumi ulioimarika wenye ushindani katika jamii.

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali imeandaa sera mbalimbali ambazo zimelenga kuhakikisha kunakuwa na maendeleo endelevu na uchumi jumuishi. “Kati ya Sera hizo ni Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 ambayo ni Sera kiongozi kwenye masuala ya kuwezesha wananchi kiuchumi, sera hiyo imeweka mikakati inayolenga kuhakikisha kwamba Watanzania wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi”.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha kitabu cha Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004 kwa Mwaka 2020/21 baada ya kuizindua katika Kongamano la Tano la Uwezeshaji Mwananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa Jengo la PSSSF Makole jijini Dodoma



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Kongamano la Tano la Uwezeshaji Mwananchi Kiuchumi baada ya kufungua kongamano hilo kwenye ukumbi wa Jengo la PSSSF Makole jijini Dodoma, Oktoba 5, 2021. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji), Geofrey Mwambe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Tano la Uwezeshaji Mwananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa Jengo la PSSSF Makole jijini Dodoma.



Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Tano la Uwezeshaji Mwananchi Kiuchumi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua kongamano hilo kwenye ukumbi wa Jengo la PSSSF Makole jijini Dodoma



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe wakati alipozindua Kanzidata ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi baada ya kufungua Kongamano la Tano la Uwezeshaji Mwananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa Jengo la PSSSF Makole jijini Dodoma, Oktoba 5, 2021. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Geofrey Mwambe na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad