HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 20, 2021

DC GONDWE AWAASA WANAOSHINDA BIKO KUZITUMIA FEDHA ZAO VIZURI KUJILETEA MAENDELEO

 


Mheshimiwa Godwin Gondwe Mkuu wa Wilaya Kinondoni, akimkabidhi mshindi wa Biko sh milioni 10 anayejulikana kama Salma Said Mohamed alizoshinda



Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mhe.Godwin Gondwe, akimkabidhi mshindi wa milioni 10 wa Biko, Salma Said, alizoshinda kwenye bahati nasibu ya Biko maarufu kama buku nibukue. Wengine pichani ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na Balozi wa Biko Kajala Masanja. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye bank ya NBC Tawi la Victoria, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu.



Mheshimiwa Godwin Gondwe kwenye miwani, akimkabidhi sh milioni 10 Salma Said alizoshinda katika bahati nasibu ya Biko. Wengine pichani ni watumishi wa bank ya NBC Tawi la Victoria na Balozi wa Biko Kajala Masanja pamoja na Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven.

…………………………………
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkuu wa wilaya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Godwin Gondwe, amewaasa Watanzania wanaoshinda bahati nasibu ya Biko maarufu kama Buku Nibukue kuzitumia fedha zao vizuri ili wakuze uchumi wao.

DC Gondwe ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya fedha jumla ya sh milioni 10 kwa mkazi wa Kijitonyama, Salma Said Mohamed, aliyeshinda katika droo kubwa ya Jumapili ikiwa ni siku chache baada ya Biko kurejesha droo kubwa sambamba na droo za papo hapo kuanzia sh 2500 hadi milioni 5 bila kusahau zaidi ya sh milioni 40 kila Jumapili.

Biko imaweza kuchezwa live kwa kuingia www.biko.co.tz pamoja na wanaotumia simu za kawaida kwa kuweka namba ya Kampuni ya 505050 na kumbukumbu 2456 huku kianzio cha kucheza kikiwa ni sh 1000 na kuendelea.

Wakati washindi wa Biko papo kwa hapo wakipatikana kila baada ya sekunde moja kwa kuchungulia nafasi kwenye gurudumua mchezo huo, wanaoshinda droo kubwa wanakabidhiwa fedha zao bank sanjali na kuwaelekeza namna bora ya kuzitumia fedha zao kwa kukuza pato lao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad