HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 8, 2021

WAWEKEZAJI VISIWANI ZANZIBAR WAHAHAKIKISHIWA USALAMA WA MALI ZAO

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la bima Zanzibar (ZIC) Arafat Haji akizungumza na Naibu Mkurugenzi  kutoka Kitengo cha uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Alhaji Mtumwa Mara baada ya kufanya Mazungumzo ya Kushirikiana kwa baina ya Taasisi hizo mbili kuhakikisha wanafikia uchumi wa blue kupitia wawekezaji wa nje na ndani na kuboresha usalama wa wekezaji kupitia bima mbalimbali.
 
 
 
 

     Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

KUELEKEA uchumi wa blue visiwani Zanzibar kupitia kwa wawekezaji Shirika la bima Zanzibar (ZIC) pamoja na Kitengo cha Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) wakutana ili kuweka mikakati ya Kushirikiana na kuweka mikakati kwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza Zanzibar

Akizungumza na Waandishi Wahabari Mara baada ya Kikao hicho cha Makubaliano baina ya pande mbili, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la bima Zanzibar (ZIC) Arafat Haji amesema Makubaliano hayo yanalenga kuweka Mikakati ya kuimarisha Mahusiano Mazuri baina ya taasisi hizi Mbili.

Haji ameongeza kuwa Makubaliano hayo yanalenga kukamata na kunufaika na fursa mbalimbali hususani kwa wenyeji na wageni wanaofanya uwekezaji visiwani hapo kuzingatia wanakata bima kwa maslahi yao pamoja Taifa Kwa ujumla.

"Mahusiano haya baina ya Shirika la bima pamoja na Kitengo cha uwekezaji kitaweza kufungua Milango mbalimbali ikiwemo wawekezaji kuongezeka kutokana na usalama wa Mali zao kuimarisha na kuboreshwa kupitia bima zetu ambazo zinalenga kusaidia hata wenye vipato duni huku swala la kutunza na kuweka usalama kwa mteja likiwa mstari wa mbele."

Hata hivyo Haji ameeleza kuwa Makubaliano hayo ni Miongoni mwa kutekeleza kauli ya Rais wa Zanzibar Dkt.Husein Mwinyi katika kutumia fursa zitokanazo na mkakati wa uchumi wa blue.
 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad