Benki ya NMB 
imetoa Sh. 60 Milioni kwa ajili ya kudhamini Mashindano Maalumu ya 
mchezo wa Gofu ya Mkuu wa Majeshi (CDF ) ambayo yanatarajia kuanza 
Septemba 17   hadi 19 kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu vya Lugalo Jijini
 Dar es Salaam.
Mashindano hayo hufanyika kila mwaka  lengo  kuu 
ni kuuinua mchezo huo pamoja na kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi 
ili kuja kuwa tegemezi siku zijazo.
Akizungumza kwenye hafla ya 
kukabidhi hundi Mkuu wa kitengo cha wateja maalumu wa NMB, Getrude 
Mallya,  alisema wanajisikia furaha kuwa sehemu ya kufanikisha kufanyika
 kwa shindano hilo ambalo anaamini mwaka huu litafana kutokana na zawadi
 nono ambazo zimeandaliwa kwa washindi.
Mallya alisema kiasi 
hicho cha fedha kimetumika katika kununua vifaa mbalimbali vitakavyo 
tumiwa na washiriki wa shindano hilo ikiwemo fulana, kofia, bendera na 
zawadi za washindi ambazo zitatolewa siku ya mwisho.
“Sisi kama 
NMB tunajisikia furaha kuona shindano la mwaka huu linakwenda kufanyika 
kwa ubora na mafanikio ya juu kabisa nahii inathibitisha kwamba sisi 
ndio Benki ambayo inaijali jamii kwa ukaribu kutokana na kudhamini 
masuala mbalimbali  ikiwo ya kimichezo,” alisema Mallya
Meneja 
huyo pia aliupongeza uongozi wa klabu ya Lugalo,  kwa imani yao kwao na 
kuendeleza mchezo wa Gofu nchini kwa juhudi kubwa wanazozifanya za 
kuanzisha mashindano mbalimbali na kuwachagua wao kushirikiana nao 
kuyadhamini.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo
 Michael Luwango, alisema zaidi ya wachezaji 170, wanatarajia kushiriki 
mashindano ya mwaka huu ikiwemo vijana wadogo wa shule (Junior) ambao 
wao ndio watakao fungua mashindano hayo siku ya kwanza  Septemba 17.
Alisema
 tofauti na miaka mingine mwaka huu wametoa nafasi ya watu mbalimbali 
kushiriki michuano hiyo wakiwemo watu binfsi na wachezaji wakulipwa 
pamoja na wageni endapo watajisikia kushiriki.
Kiongozi huyo 
alisema mpaka sasa mwitikio kwa watu wanaoomba kushiriki ni mkubwa 
ambapo zaidi ya watu 100 wameshathibitisha ushiriki wao na maandalizi 
yanakwenda vizuri ikiwemo ubora wa viwanja ambavyo vitatumika kwenye 
shindano hilo.
Naye Katibu wa Chama cha Gofu Tanzania Boniface 
Nyiti, alisema shindano hilo la Mkuu wa Majeshi lipo kwenye kalenda ya 
TGU na limekuwa na mchango mkubwa kwa taifa kutokana na kutoa wacheaji 
wengi ambao wanajenga timu ya taifa.
Nyiti aliwataka viongozi wa 
klabu za mchezo huo wanaoanzisha mashindano mengine kipindi ambacho 
shindano la Mkuu wa Majeshi linafanyika watawachukulia hatua ikiwemo 
kuwafungia kutoshiriki mchezo huo kwa kufuata sheria kwani kufanya hivyo
 nikuwanyima fursa wachezaji kuto onesha uwezo wao.
Mpaka sasa 
zaidi ya klabu 10 kutoka mikoa tofauti imethibitisha kushiriki michuano 
hiyo baadhi yao ni Morogoro, Zanzibar, Arusha, Moshi, Dar es Salaam 
Gymkhana Klubu na Lugalo .
 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum Benki ya NMB, Getrude Mallya 
akimakabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh.milioni 25.5 Mwenyekiti 
wa Klabu ya Golf ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo 
ikiwa ni udhamini wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 
'NMB CDF Trophy 2021'. Kulia ni Meneja wa Club ya Golf ya Lugalo, Luteni
 Kanali, Frank Kaluwa na Meneja Mwandamizi Wateja Maalum wa NMB, 
Emmanuel Mahodanga wakishuhudia. Benki ya NMB imetoa takribani milioni 
60 kwa ajili ya udhamini wa mashindano hayo kiujumla kwa mwaka huu.
Mkuu
 wa Kitengo cha Wateja Maalum Benki ya NMB, Getrude Mallya (katikati) 
akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye hafla ya kupokea mfano
 wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 25.5 kwa ajili ya udhamini 
wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF Trophy 
2021'. Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo, Brigedia Jenerali
 Mstaafu Michael Luwongo pamoja na Meneja Mwandamizi Wateja Maalum wa 
NMB, Emmanuel Mahodanga (kulia) wakishuhudia.
 

No comments:
Post a Comment