HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 10, 2021

WAJUMBE WA KONGAMANO LA MISRI WAKUBALIANA KUKUZA UCHUMI LICHA YA COVID 19

Na. Josephine Majula, WFM – Cairo Misri

Wajumbe wa Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri (Egypt International Cooperation Forum) ikiwemo Tanzania wamekubaliana kutoa ripoti ya tathimini ya mkutano huo baada ya miezi mitatu ambapo yote yaliyojadiliwa na kukubaliwa likiwemo suala la kuendeleza ukuaji wa uchumi licha ya changamoto ya Covid 19 yatatolewa mwongozo kwa ajili ya utekelezaji.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba wakati wa kuhitimisha Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri (Egypt International Cooperation Forum) lililofanyika kwa siku mbili mjini Cairo nchini Misri.

Dkt. Mwigulu alisema kongamano hilo limemalizika na ajenda mbalimbali zilijadiliwa zikiwemo za mikakati ya kupambana na Uviko- 19 na umuhimu wa mahusiano ya kimataifa katika kujijenga kiuchumi.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwigulu alitembelea ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Misri ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Misri Mhe. Meja Jenerali Anselm Bahati.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Daniel Sillo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban na wataalamu kutoka wizara hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri lililofanyika Cairo Misri.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri lililofanyika Cairo Misri.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Balozi wa Tanzania nchini Misri Mhe. Meja Jenerali Anselm Bahati, baada ya Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri lililofanyika Cairo Misri.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, akiteta jambo na Balozi wa Tanzania nchini Misri Mhe. Meja Jenerali Anselm Bahati, baada ya Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri lililofanyika Cairo Misri.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo, akiteta jambo na Balozi wa Tanzania nchini Misri Mhe. Meja Jenerali Anselm Bahati, baada ya Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri lililofanyika Cairo nchini Misri.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Misri Mhe. Meja Jenerali Anselm Bahati (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo, alipotembelea ofisi za ubalozi Cairo nchini Misri.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ubalozi nchini Misri alipotembelea ofisi na kufanya kikao cha ndani.  Wa nne kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Meja Jenerali Anselm Bahati  na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango - Misri)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad