HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 23, 2021

NIC YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WA LADY FATIMA KIGAMBONI

  

Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC,) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Lady Fatima Kigamboni jijini Dar es Saalam.

Meneja  Uhusiano wa NIC Karimu Meshack (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo wa vyakula katika kituo cha Lady Fatima na kueleza kuwa NIC itaendelea kutekeleza sera ya shirika hilo kwa kurudisha kwa jamii, kulia ni msimamizi wa kituo hicho Omary Kalekela, leo jijini Dar es Salaam.

Meneja  Uhusiano wa NIC Karimu Meshack (wa pili kushoto) akikabidhi sehemu ya vyakula vilivyotolewa na shirika hilo kwa msimamizi wa kituo hicho Omary Kalekela (kushoto,) leo jijini Dar es Salaam.


SHIRIKA La Bima la Taifa (NIC,) limetembelea na kutoa msaada wa vyakula katika kituo cha kulea watoto yatima cha Lady Fatima kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera kurudisha kwa jamii inayoyekekezwa na shirika hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Meneja Uhusiano kutoka NIC Karimu Meshack amesema sera ya shirika hilo ni kurudisha kwa jamii kwa faida wanayoipata na hiyo ni pamoja na kusaidia miradi ya Serikali inayogusa jamii moja kwa moja hasa watoto, wanawake na wazee.

Karimu amesema, baada ya kuona uhitaji wa chakula katika kituo hicho wakaona ni vyema kuungana na kituo hicho kinacholea watoto yatima wapatao 25.

"NIC daima tupo karibu na jamii, na leo tumekuja kuwatembelea watoto wetu na kuwaletea mahitaji yatakayosaidia katika ukuaji wa watoto hawa...Tumeleta mahitaji mbalimbali  ikiwemo unga wa sembe na ngano, mchele, maharage na mafuta ya kupikia." Amesema.

Aidha amesema, Shirika hilo lipo pamoja na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma za msingi ikiwemo afya na elimu zinawafikia wananchi.

Kwa upande wake mwanzilishi wa kituo hicho Omary Kalekela ameishukuru NIC kwa kuwatembelea na kutoa msaada wa vyakula kwa watoto hao na kuwakaribisha wadau wengine kufuata nyayo za NIC katika kushiriki kuwalea watoto hao kwa namna mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad