Na Anthony Ishengoma Ishengoma-Shinyanga
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga amesema kuzimika kwa taa za Barabarani katika
Manispaa ya Shinyanga kulileta sintofahamu kwa wananchi wa Shinyanga
kutokana na athari za usalama wa biashara zao ulichangiwa na uwepo wa
wahalifu waliotumia fursa ya kuzimika kwa taa hizo kufanya uhalifu.
Taa
hizo za barabarani zilizimika kutoka na mkandarasi hapo awali kufunga
taa za kutumia nguvu ya jua ambazo zilikuwa hazina ubora na kuzimika kwa
kipindi kifupi baada ya kuwa zimefungwa na kuleta usumbufu kwa katika
mitaa kwani biashara zilikuwa zinafungwa mapema saa kumi na mbili.
Akiongea
na vyombo vya habari wakati wa zoezi la kufunga upya taa hizo Dkt.
Philemon Sengati alisema uongozi katika Mkoa wa Shinyanga ulimtaka
mkandarasi huyo kufanya marekebisho katika taa hizo na alikubali sharti
hiyo na kwa kipindi kifupi sasa tayari taa zimeanza kufungwa.
‘’Wafanyabiashra
katika eneo hili walilazimika kukodi taa kwa takribani elfu 15 kwa
mwezi zile zenye mwanga mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara baada ya taa
za wali kuzima na palikuwa na sintofahamu’’. Aliongeza Dkt. Philemon
Sengati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Dkt. Sengati aliongeza kuwa
taa zilizokuwa hazifanyi kazi ni taa 428 ambazo mkandarasi amezifanyia
marekebisho na amefanya hivyo kwani bado alikuwa anadai kiasi cha Tsh.
Mil.200 ambazo aliambiwa kama atashindwa kusimamia zoezi hilo basi Mkoa
usingetoa kiasi hicho cha fedha kama sehemu ya deni kwa mkandarasi huyo.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko alilitaja zoezi hilo
kuwa sehemi muhimu la kiusalama kwani baadhi ya vibaka walikuwa
wanatumia fursa ya giza kuleta usumbufu kwa wananchi ikiwemo
wafanyabiashara wa mtaa wa sukari ambao walikuwa wanalazimika kufunga
biashara mapema kuepuka usumbufu huo.
‘’Kikubwa walitakiwa
kurudia taa zote 428 na mpaka sasa washabadilisha taa 400 na tunategemea
leo watamaliza taa zilizobaki na wamekuwa wakibadilisha taa 60 kwa siku
kwahiyo niseme wananchi wanaweza kufanya biashara zao usiku kucha kama
wanaweza na wale wengine ambao walikuwa wanapata usumbufu mkubwa
kutokana na taa kuzimika na wao wanaweza kuendelea na biashara zao’’.
Aliongeza Bi. Jasinta Mboneko.
Baadhi ya Wananchi walipongeza
hatua ya kurejesha tena taa hizo akiwemo Bi. Irene Mathias ambaye
alisema kuwa kitendo cha taa hizo kuwaka sasa ataendesha biashara yake
mpaka usiku lakini pia wasiwasi wake aliokuwa nao kuhusu kukabwa na
vibaka haupo tena.
Wakati huohuo Msimamizi wa Tarura Mkoa wa
Shinyanga Muhandisi Osward Girbert alikiri kuzimika kwa taa hizo na
changamoto za kimkataba lakini sasa taa izo zimewaka na mkandarasi
alilazimika kufanya marekebisho kwa kuagiza betri mpya na hivyo
kurejesha huduma hiyo na hivyo anashukru kurejea kwa huduma hiyo.
Mfanyabiashara
ndogo aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Cyprian alisema kabla ya
marekebisho ya Taa alikuwa hawezi kufanya biashara yake kwa kipindi
kirefu kwani alikuwa anatumia taa za kuchaji lakini sasa kutokana na
kuwepo kwa mwanga wa kutosha ataweza kufanya biashara kutegemea mwanga
wa Taa hizo na hivyo kufanya biashara yake vizuri.
Benki ya Dunia
ilitoa msaada wa kujenga mtandao wa Barabara za lami Manispaa ya
Shinyanga takribani kilomita 13 na serikali kupitia Tarura iliweka
mkandarasi kufunga taa ambazo awali zilizimika kutokana na betri
kutokuwa na ubora lakini zoezi linarudiwa ili kuleta ufanisi kati suala
zima la kuhakikisha taa za barabarani zinarejea katika hali yake.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akifuatilia kwa makini kujionea namna ambavyo mafundi wa kutenegeneza taa za barabarani za umeme jua namna zunavyofanyakazi kutoka kwa moja ya mafundi wa kazi hizo jana katika mitaa ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akifuatilia kwa makini akipata ushauri kutoka kwa Meneja wa Tarura Shinyanga Muhandisi Salvatory Amri wakati zoezi la kubadilisha taa za barabarani jana katika mitaa ya Manispaa ya Shinyanga pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akifuatilia kwa makini akipata ushauri kutoka kwa Meneja wa Tarura Shinyanga Muhandisi Salvatory Amri wakati zoezi la kubadilisha taa za barabarani jana katika mitaa ya Manispaa ya Shinyanga pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko.
No comments:
Post a Comment