HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 15, 2021

DC Mayanja awaomba viongozi wa dini kusimamia makuzi

 


 

Na John Walter-Hanang
Mkuu wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja amewaomba viongozi wa dini wilayani hapo  kuendelea kusimamia malezi na makuzi ya Vijana ili kuwa na Taifa lenye hofu ya Mungu, Uadilifu na Uzalendo.

Ametoa ombi hilo katika mkutano wa 45 wa  Mwaka wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Mbulu uliofanyika Wilayani hapo ambapo  amewashukuru  na kulipongeza kanisa hilo kwa huduma nzuri wanazotoa katika hasa  katika huduma za Afya na Elimu kwani wanaunga jitihada za  Selikali kwa vitendo.

Aidha amewahakikishia Serikali ya Wilaya itaendelea kutoa ushirikiano kwao ili kufikia malengo ya kanisa.

Mkutano huo uliongozwa na Baba Nicolaus Nzangazelu  wa Dayosisi  ya Mbulu  Nicolaus   na kusimamiwa na Baba Askofu  Michael Adam wa Dayosisi ya Mara na Watumishi wa Mungu zaidi ya 300 kutoka Wilaya za Mbulu, Hanang,Babati  na Wilaya za jirani.

Baba Askofu  Nicolaus Nzangazelu  amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kushiriki katika Mkutano huo na ameahidi kushirikiana na Serikali ya Wilaya katika kuimairisha huduma za jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad