HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 18, 2021

WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUJIFNYA WATUMISHI WA SHIRIKA LA UMEME (TANESCO) MKOANI ARUSHA

 


Na. Abel Paul Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP-JUSTINE MASEJO leo tarehe 18.08.2021ametoa taarifa kwa  vyombo vya habari na amesema  kuwa tarehe 17.08.2021  muda wa 09:00 Alasiri katika ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Arusha zilizopo katika mtaa wa Old line kata ya Themi halmashauri ya Jiji la Arusha, Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifanikiwa kuwakamata watu watatu ambao ni GIDIONI WILLIAM miaka 26 mkazi wa Sombetini, RICHARD FRANK  miaka 20 Mkazi wa Daraja la II, GODSON ERICK miaka 20 Mkazi wa Moshono wakijifanya watumishi wa Shirika la Umeme (Tanesco) Mkoa wa Arusha.

ACP- MASEJO amesemakuwa Watuhumiwa hao walikamatwa mara baada ya kupokea taarifa toka kwa raia wema kwamba, wamekuwa wakijihusishsa na wakuwadanganya wananchi ambao wanahitaji huduma za kuunganishiwa umeme kuwa wao ni Maofisa wa Shirika hilo na wana uwezo wa kuwapatia huduma wanazozihitaji kwa njia ya mkato, ndipo timu ya makachero wa Polisi wakirikiana na maofisa wa shirika la umeme waliweka mtego na kufanikisha kuwakamata watuhumiwa hao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha amesema kuwa  Kutokana na tuhuma hizo Jeshi la Polisi Mkoani hapa tunaendelea kuwahoji watuhumiwa ili kupata mtandao mzima unaohusika na vitendo hivyo vya kitapeli katika ofisi za shirika la umeme (Tanesco) Mkoa wa Arusha.

Ameendelea kusema kuwa pindi upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi  kuzitumia ofisi na taasisi za umma ambazo zipo kwa ajili yao pindi wanapohitaji huduma yoyote hali hii itasadia kuwakwepa walaghai ambapo wanaweza kuwaingiza katika matatizo au hasara. Aidha naendelea kuwaomba wananchi wa mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP-JUSTINE MASEJO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad