Wanachama
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wamefanya uchaguzi wa
viongozi wapya wa tawi ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano
uliofanyika leo katika ukumbi wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Nafasi
zilizogombaniwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Tawi ,Katibu wa Tawi,
Mwenyekiti wa Wanawake, Katibu wa wanawake, Mjumbe wa Vijana, mjumbe wa
kundi la watu wenye ulemavu na wajumbe wa Halmashauri ya Tawi.
Awali
akifungua mkutano huo, Afisa Tawala Mwandamizi kutoka TCAA, Patrick
Vyamana ameupongeza uongozi uliopita wa TUGHE kwa kazi nzuri
walioifanya katika kudumisha mahusiano mazuri kati ya menejimenti na
chama hicho na pia amewasihi wanachama kushiriki katika shughuli za
chama Ili chama kiendelee kuwa hai na kutekeleza majukumu yake.
Vyamana
amewaeleza wajumbe waliohudhuria mkutano huo kuzingatia sheria wakati
wa uchaguzi na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki ili
kuepusha migogoro na kutoa ahadi ya ushirikiano kwa uongozi mpya
utakaochaguliwa katika kutatua changamoto zilizopo na kuendelea
kusisitiza katika kudumisha mshikamano na kutoa ushirikiano kwa
viongozi wapya watakaopatikana.
``Mchakato
huu ni huru na wa haki, halali, na wa kidemokrasia tunahakikisha
tunatekeleza jukumu hili, tukizingatia demokrasia kuepusha migogoro na
baada ya uchaguzi tukubali matokeo na tutoe ushirikiano kwa
watakaoshinda.``. Amesema Vyamana.
Kwa
upande wa msimamizi wa uchaguzi ambaye ni katibu wa TUGHE Mkoa wa Ilala
Bi. Sarah Rwezaula wakati akitangaza matokeo amewapongeza wajumbe wote
ambao wamejitokeza kuwania nafasi hizo na kuwataka wanachama kuwapa
ushirikiano viongozi wapya.
Katika
uchaguzi huo Bi Jackline Ngoda ameibuka kidedea kwenye nafasi ya
Uenyekiti wa tawi kwa kupata kura 39, huku nafasi ya Katibu ikichukuliwa
Shukuru Mhina ambaye amepata Kura 51.
Viongozi hawa wapya wa TUGHE ) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wataongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Afisa Tawala Mwandamizi kutoka TCAA, Patrick Vyamana akizungumza na wajumbe wa TUGHE tawi la TCAA wakati wa ufunguzi wa uchaguzi
wa viongozi wapya wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya
(TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) uliofanyika
katika ofisi zake zilizopo mkoani Dar es Salaam leo.
Msimamizi
wa uchaguzi ambaye ni Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Sarah Rwezaula
akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wapya wa
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya
Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) uliofanyika katika ofisi zake zilizopo
mkoani Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamis Kisesa aliyemaliza muda wake akisoma risala kabla
ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wapya wa Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la TCAA uliofanyika katika ofisi zake
zilizopo mkoani Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wajumbe Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakifuatilia zoezi la uchaguzi wa viongozi wa TUGHE tawi la TCAA uliofanyika katika ofisi za mamlaka hiyo leo mkoani Dar es Salaam.
Zoezi la Uchaguzi likiendelea
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
Uongozi mpya wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waalikwa mara baada ya
kumalizika kwa uchaguzi huo iliofanyika leo katika ukumbi wa Mamlaka
hiyo mkoani Dar es Salaam.
Uongozi wa zamani wa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waalikwa mara baada ya
kumalizika kwa uchaguzi huo iliofanyika leo katika ukumbi wa Mamlaka
hiyo mkoani Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment