SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KUSIMAMIA, KUDHIBITI NA KURATIBU MAPATO NA MATUMIZI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 16, 2021

SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KUSIMAMIA, KUDHIBITI NA KURATIBU MAPATO NA MATUMIZI

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara, George Simbachawene, akizungumza katika kikao cha kupitia taarifa ya Kamati hiyo kwa robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha 2020/2021, kilichofanyika jijini Dodoma, leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, na kulia ni Katibu wa Kamati, Jenitha Ndone.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara, George Simbachawene (kushoto), akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuongoza Kikao cha Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo.

Mjumbe wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Emmanuel Kayuni, akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (hayupo pichani), katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika jijini Dodoma, leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara, George Simbachawene (wapili kulia), akimsikiliza Mjumbe wa Kamati hiyo, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza alipokuwa akifafanua jambo katika Kikao cha kupitia taarifa ya Kamati hiyo kwa robo ya kwanza na ya tatu ya Mwaka wa Fedha 2020/2021, kilichofanyika jijini Dodoma, leo. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, na kulia ni Katibu wa Kamati, Jenitha Ndone.

Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad