Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bashir Muhoja akiwa ameushika mwenge wa Uhuru ambao ulikuwa unakagua na kufungua miradi ya kimaendeleo katika Halmashauri hiyo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nyerere wakiwa wameshiriki kuupokea mwenge wa Uhuru ulipokuwa umewasili katika shule hiyo kwa ajili ya kuzindua klabu ya PCCB
Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bashir Muhoja,ayefuta ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo katikati ni kiongozi wa kukikmbiza mwenge wa Uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwampashi anayefuta na Meya wa manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada na wa mwisho kulia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Costatino Kihwele
Kikundi cha hamasa kikiburudisha wakati wa mwenge wa Uhuru
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MWENGE wa Uhuru umepongeza miradi ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa kutokana na kuwa na ubora unaolingana na thamani ya miradi na kusaidia kuchochoe maendeleo kwa wananchi wanaokusudiwa katika kukuza uchumi wan chi.
Akizungumza wakati wa kutembelea na kugagua miradi hiyo mkimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwampashi Alisema kuwa wameridhishwa na miradi waliyoitembelea wakati wa mwenge wa Uhuru ulipokuwa katika Halmashauri hiyo.
Mwampashi alisema kuwa wamejionea mradi mzuri wa wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa kupambana na rushwa unaotekelezwa katika shule ya sekondari ya Nyerere iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa ambao unalenga moja kwa moja kuendelea na mapambano dhidi ya rushwa kuanzia shuleni.
Alisema kuwa kwa sasa kuna vijana wengi ambao wanatakiwa kuendelea kupata elimu ya kupambana na rushwa ili hapo baadae kuwe na kizazi ambacho kitakuwa kinajua madhara ya kupokea au kutoa rushwa.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo Mwampashi alisema kuwa mradi wa kilimo uliopo katika kijiji cha Kising’a umekuwa mradi bora kati ya miradi ya mwenge ambayo imetembelea kwa kuwa unamanufaa makubwa kwa wananchi wanaouzunguka mradi huo na wale waliopo nje ya mradi huo.
Alisema kuwa wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa wanatakiwa kula mlo kamili ili kupunguza na kuondoa kabisa tatizo la utapiamlo na udumavu kwa watoto wadogo kwa kuwa wanaardhi ambayo inafaa kwa kilimo cha aina yoyote ile.
Awali akisoma taarifa ya mradi wa kilimo cha mboga mboga na matunda katika kijiji cha kising’a ,afisa ugani wa kata ya kising’a Stanley Mwengilolo alisema kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi 87,705,000 ambacho ndio kinatekeleza mradi huo mkubwa wenye manufaa makubwa kwa wananchi wa kata hiyo na nje ya kata hiyo.
Mwingilolo alisema kuwa mradi huo kwa kiasi kikubwa umefanikishwa na uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kuanzia ngazi ya awali hadi ulipo fika kwa lengo la kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo.
Alisema kuwa mradi huo umekuwa mfano wa kuigwa kwa wananchi wote wanaopenda kilimo cha mboga mboga na matunda kwa kulima kilimo cha kisasa ambacho kimekuwa na faida kwa wananchi wanaolima kilimo hicho.
No comments:
Post a Comment