Mkuu wa mkoa wa
Pwani Mhe Abubakar Kunenge leo Agosti 11, 2021 majira ya saa 12 Asubuhi
amepokea Mwenge huo kutoka kwa Mhe. Martine Shigela Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, Kunenge Ameeleza kuwa Mwenge huo ukiwa Mkoani hapo
utakimbizwa katika Wilaya saba za Mkoa huo na kufikia Miradi 87 ambapo
Miradi 18 Itafunguliwa Miradi 9 Itawekwa mawe ya Msingi na Miradi 60
Itakaguliwa.
Miradi yote inathamani ya Shilingi 57,311,572,720.
Ameeleza Miradi yote imezingatia Kauli Mbiu ya Mbio Maalumu za Mwenge
wa Uhuru 2021 Isemayo TEHAMA ni Msingi waTaifa Endelevu itumie kwa
usahihi na Uwajibikaji.
Baada ya kupokea Mwenge huo Mhe Kunenge amekabidhi kwa Mhe Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Abdalah.
"Kwa
niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Pwani, ninayoheshima kubwa kuwakaribisha
wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mkoani Pwani na kwa kipindi chote
Mjiskie mpo Nyumbani kwa ndugu zenu wakarimu Wanapwani.
No comments:
Post a Comment