Na Amiri Kilagalila,Njombe
Umoja
wa wakulima wa zao laparachichi na kilimo hai kupitia asasi yao ya
Njombe southern Highland delepment Association NSHDA mkoa wa Njombe
wamedhamiria kupanua wigo wa uzalishaji wa zao hilo kwa kuwataka
wawekezaji kufika mkoani Njombe kuwekeza,ambapo asasi hiyo itachukua
jukumu la kusimamia mashamba yao kuanzia kumiliki shamba mpaka uvunaji
wa tunda hilo.
Programu
hiyo inalenga kupokea wawekezaji mbalimbali wenye nia ya kuwekeza katika
kilimo cha parachichi na Makademia ambao watakuwa chini ya usimamizi wa
asasi hiyo ya NSHIDA inayowahakikishia upatikanaji wa mashamba na
usimamizi hadi msimu wa mavuno lengo ni kuongeza uzalishaji maradufu
zaidi ya sasa kutokana na uhitaji mkubwa waparachichi katika soko la
dunia.
Aidha hatua hiyo
imechukuliwa kutokana na wakulima wengi kukosa utaalamu wa kilimo licha
ya kuwa na nia ya kuwekeza ambapo asasi hiyo chini ya mkurugenzi wake
Frank Msigwa imelazimika kuzindua mfumo wa kusimamia mashamba ya
wakulima kuanzia hatua ya awali hadi mavuno kwa gharama ndogo.
“Kutokana
na uhitaji mkubwa sana wa parachichi na Makademia duniani tumeona
tuanzishe hii program ili tuweze kuwasaidia watanzania wenzetu na wasio
watanzania wanaopenda kuwekeza kwenye zao hili ili tuweze kujitosheleza
soko kwasababu sasa hivi matunda yamekwisha na soko limefunguka,wanunuzi
wanakuja na mamilioni ya pesa na kurudi nayo kwasababu matunda hakuna
ila Njombe tuna ardhi ya kutosha”alisema Frank Msigwa
Baadhi
ya wakulima wa parachichi mkoani Njombe akiwemo Godfrey Nyagawa na
Lusi Zabron wamepongeza kuanzishwa kwa mfumo huo wa kuwasaidia wakulima
wanao vutiwa kuwekeza katika kilimo cha parachichi huku wakisema
utasaidia kukuza uchumi wa familia na mkoa kwa ujumla kutokana na
uhitaji mkubwa wa parachichi kwa sasa.
“Program
hii itasaidia sana kukuza uchumi kupitia kwenye kilimo hiki hususani
kwenye familia lakini pia itaongeza uzalishaji wa zao hili kwa kufanya
matunda yaongezeke kwa wingi kwasababu hayatoshelezi kwa sasa”alisema
Godfrey Nyagawa
Baadhi ya
Vijana Ambao wamejiajiri kwenye kilimo cha zao la Parachichi
amewaasa vijana waache kulalamika juu ya ugumu wa maisha bali
wachangamkie fursa mbalimbali zilizopo kwenye maeneo yao ikiwemo
kuwekeza kwenye kilimo hicho
“Fursa
kwenye hiki kilimo zimekuwa ni kubwa niwashauri vijana wenzangu
kuwekeza kwenye hiki kilimo kwasababu mtaji ni mdogo kwa kuwekeza miche
michache michache na hata kama kuna changamoto basi NSHIDA wameleta huu
mpango ambao unaweza ukawekeza kwa kusimamiwa nao kwasababu wao wana
uzoefu wa kutosha”alisema mmoja wa kijana aliyewekeza kwenye kilimo
hicho.
No comments:
Post a Comment