Na Humphrey Shao,Michuzi TV Dar es Salaam
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto .Prof. Abel
Makubi, amezindua zoezi la usambazaji wa chanjo ya UVIKO 19 aina ya
Jonson Jonson Kwenye BOHARI ya Dawa (MSD) iliyopo Keko Jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada uzinduzi
huo Prof .Makubi amesema chanjo hizo zitasambazwa katika mikoa yote
26 ya Tanzania Bara.
"Chanjo hizi ni Bure na zitapatikana
katika Hospitali zote zitakazo elekezwa za Serikali na zile za Binafsi
ambazo zitakuwa zimeteuliwa" Amesema Prof Makubi.
Amesisitiza
kuwa chanjo hiyo ni Bure na Serikali imesambaza katika mikoa yote kwa
idadi tofauti kulingana na visa vilivyoripotiwa katika mkoa huo.
Ametaja
kuwa chanjo hii inaanza kutolewa kwa makundi maalum ambayo ni Wazee
,Watumishi , Watumishi wa majeshi na Wenye magonjwa hatarishi.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Dr.Benjamini Hubila amesema
mchakato wa usambazaji umekamilika na shirika lake limejipanga vyema
kupeleka chanjo hizo kwa wakati.
Amesema MSD itasambaza chanjo hizo ndani ya siku Saba kwa kupitia mtandao wake wa usambazaji dawa nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Prof.Abel Makubi akikabidhi chanjo kwa Mkurugenzi wa MSD Dr.Benjamini Hubila.Wafanyakazi wa MSD wakifungua majokofu yanayotumika kuhufadhia chanjo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Prof.Abel Makubi akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa usambazaji wa chanjo ya uviko 19 .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD nchini, Dr.Benjamini Hubila akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment