RAIS SAMIA APOKEA NDEGE MPYA AINA YA BOMBADIER DASH 8-Q400 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 30, 2021

RAIS SAMIA APOKEA NDEGE MPYA AINA YA BOMBADIER DASH 8-Q400

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kupokea Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021. Wa pili kushoto ni Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na wa tatu kulia ni waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasalimia Wananchi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumuunga Mkono kwenye mapokezi ya Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kupokea Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021. IKULU.
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad