WAZIRI WA VIWANDA ATEMBELEA BANDA LA UTT AMIS SABASABA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 6, 2021

WAZIRI WA VIWANDA ATEMBELEA BANDA LA UTT AMIS SABASABA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (kulia), akisaini kitabu cha wageni alipofika katika banda UTT AMIS lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF). Katikati ni Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya UTT AMIS, Martha Mashiku.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya UTT AMIS, Martha Mashiku, juu ya fursa za uwekezaji zinazopatikana katika kampuni hiyo.

Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Martha Mashiku, akitoa maelezo kuhusu fursa zilizopo katika mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kwa mwananchi aliyefika katika banda la kampuni hiyo kwenye Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Waziri Ramadhani, akitoa vipeperushi vya taarifa za fursa zilizopo katika mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Temboni waliotembelea banda la kampuni hiyo kwenye Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad