HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 6, 2021

TMDA KUPUNGUZA ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

 Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

KATIKA kupunguza ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza, serikali imeweka mkakati katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa elimu kuhusu matumizi ya tumbaku.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maonesho ya 45 ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere 'Sabasaba' , Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Gaudensia  Simwanza amesema kuanzia Julai Mosi mwaka huu mamlaka yao imepewa jukumu kuhakikisha wananchi wanapatiwa elimu.

Simwanza amesema, matumizi ya tumbaku ni kwa kuweka, kunusa au kutumia kwa njia yoyote ni kosa kisheria na katika kanuni inakataza kutumia tumbaku.

"Serikali imeamua kuweka mkazo huo kutokana na ongezeko la magonjwa yasiyo yakuambukiza yanayotokana na matumizi makubwa ya tumbaku na eneo kubwa limekuwa linasababishwa nalo", amesema Simwanza.

Aidha, amewataka wamiliki wa kumbi za starehe kufika katika ofisi zao ili kupata elimu zaidi ya matumizi ya tumbaku katika maeneo yao ya biashara.

Simwanza amesema, TMDA imeweka kipaumbele katika kuhakikisha  inatoa elimu kwa wananchi kupitia katika banda lao lililopo ndani vya Viwanja vya Maonesho ya Mwalimu Nyerere ili kuweza kupata elimu zaidi.

Hata hivyo, Simwanza amemalizia na kusema TMDA imejipanga kutoa elimu kwa wananchi wote kwani matumizi ya tumbaku si sahihi na kosa kisheria.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Gaudensia  Simwanza akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maonesho ya 45 ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad