Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile akizungumza jambo ndani ya Banda la TTCL alipotembelea kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 kujionea huduma na bidhaa mbalimbali za shirika hilo.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Ramadhani Mshana mara baada ya kutembelea kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 kujionea huduma na bidhaa mbalimbali za TTCL kwenye maonesho hayo.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile (kushoto) akizungumza na baadhi ya wanahabari mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile akijionea huduma ya mikutano kwa njia ya video 'Video conference' inavyofanya kazi alipotembelea kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 kujionea huduma na bidhaa mbalimbali za TTCL kwenye maonesho hayo.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile akisaini kitabu cha wageni ndani ya Banda la TTCL alipotembelea kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 kujionea huduma na bidhaa mbalimbali za TTCL.
Meneja Masoko wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Janeth Maeda (kulia) akiwahudumia wateja walotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wateja walotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam wakipata huduma mbalimbali.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kuja na bidhaa za ubunifu zinazojibu changamoto za maambukizi ya virusi vya corona. Waziri Dk. Ndugulile ameyasema hayo, Katika banda la TTCL kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam alipotembelea kujionea bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL.
Alisema TTCL na Kituo cha Taifa cha Intaneti (NIDC) imekuja na mfumo wa ukusanyaji wa fedha katika baadhi ya mageti na huduma kwa kutumia kadi za kitaifa za kutunzia fedha na kufanya miamala inayojulikana kama ‘N-Card’ inayofanya kazi kwa katika Kivuko cha Feri Kigamboni na kwenye viingilio vya mchezo wa mpira wa miguu kwa baadhi ya viwanja.
Aliongeza kuwa Shirika la TTCL pia limeleta huduma ya kufanya mikutano kwa njia ya video 'Video conference' huduma ambayo inawawezesha watu kufanya mikutano yao bila kulundikana eneo moja, ambapo inajibu changamoto ya mikusanyiko hasa kipindi hiki cha tishio la ugonjwa hatari wa virusi vya Corona.
Alisema matumizi ya ‘N-Card’ yanaondoa utaratibu wa awali wa malipo ya ‘cash’ kwa kulipa papo hapo hususan katika maeneo yenye misongano ya malipo kama katika viingilio uwanjani, baadhi ya mageti na hata kwenye matamasha utaratibu ambao ni hatari hasa kipindi hiki ambacho mikusanyiko na misongamano isio ya lazima haitakiwi kwa kile kuchukua tahadhari ya virusi vya corona.
Kwa upande wake, Meneja wa Banda la TTCL, Ramadhani Mshana akizungumza ndani ya banda lao alizitaka taasisi binafsi na za Umma zinzohitaji kupatiwa huduma mpya za call center kutembelea banda la TTCL kupata suluhisho hilo pamoja na huduma zingine kama vile 'Video conference' (Mkutano kwa njia ya Video), Kuunganisha wateja wa simu na intaneti kwa njia za Copper, Fiber, na Microwaves (Radio).
Alibainisha kuwa bidhaa zingine zinazopatikana ndani ya banda la TTCL ni pamoja na Vifaa vya wireless internet kama MiFi, Router, Dongle, Wingle Simu za mezani za Wireless maarufu kama FWT Router mpya ya kisasa kabisa ambayo ina uwezo wa kuunganishwa na simu ya mezani (kichwa cha simu).
Aliongeza kuwa huduma zingine zinazotolewa ndani ya banda la TTCL, ni pamoja na kutoa bure line za simu (Simcard) kwa wateja zikiwa na MBs na dk na sms za kutosha kwa matumizi ya wiki nzima bure.
No comments:
Post a Comment