Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) Jenista Muhagama ameliagiza Shirika la Nyumba la Watumishi Hosing (WHC) kushirikisha Taasisi zingine za umma zinazotoa huduma muhimu kwa Jamii ili kupunguza gharama za maisha kwa wapangaji.
Waziri Jenister alitoa agizo hilo Dar es Salaam,jana baada ya kutembelea mradi wa nyumba 65 za Shirika hilo zilizojengwa maeneo ya Bunju B na kubaini changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa barabara na shule.
Alisema mradi mkubwa kukosa huduma muhimu sio jambo zuri kwani inawapa changamoto wahitaji kwenda kutafuta huduma hizo mbali badala ya kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi.
“Naagiza kwa viongozi wa watumishi housing katika miradi mingine mikubwa inayokuja lazima tushirikishe na mamlaka zingine za kutoa huduma muhimu kama maji barabara na huduma zingine kama zahanati na shule ziwe karibu kwa sababu uhitaji unakuwa makubwa",alisema Jenista
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kutembelea Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa (kushoto) akizungumza aki akitoa maelekezo kuhusu mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama, (katikati) akiwa ameambatana na watendani mbalimbali wakitembelea Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
No comments:
Post a Comment