Naibu Waziri wa Nishari Mhe. Wakili Stephen Byabato amesema, jumla ya
vijiji 192 kati ya vijiji 524 vilivyopo mkoani Lindi,vinakwenda kupatiwa
huduma ya umeme,baada ya kuzinduliwa kwa Mradi Kabambe wa Kusambaza
Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika mkoa wa Lindi.
Ameyasema hayo tarehe 03 Julai, 2021 alipokuwa akifanya uzinduzi wa
Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika
kijiji cha Narungombe, Wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.
Amesema
Serikali ya Awamu ya sita inayo azma madhubuti kabisa ya kuhakikisha
watanzania wote wanapata umeme kwa ajili ya kufanya shughuli za kijamii
pamoja na za kiuchumi na kuwa umeme huo unaletwa na Serikali kwa
asilimia mia moja.
Amewataka wakandarasi kutekeleza mradi huo
kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na miradi ambayo serikali
inatekeleza kwa ajili yao.
Amewaomba wananchi kutumia fursa
hiyo ya kujiunganishia umeme utakapokuwa tayari na kuwa kwa sasa waanze
kutandaza nyaya kwenye nyumba zao ili kujiandaa na fursa iliyojitokeza
ya kuunganishiwa umeme.
Amewaomba wananchi kuitunza miundombinu
ya umeme ili idumu kwa kuacha tabia ya kuchoma moto maeneo yenye nguzo
za umeme kwani Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa katika kuweka
miundombinu ya umeme kwenye maeneo yao kwa lengo la kuwanufaisha
wananchi.
Naibu Waziri Byabato, amewataka watumishi wa TANESCO
kuwachukulia hatua wale watakaobainika kuhujumu miundombinu hiyo ya
umeme.
Aidha Mh. Byabato, amemuagiza Meneja wa TANESCO mkoa wa
Lindi Mha. Kainda Museru Kuhakikisha anahamishia ofisi ya malipo
vijijini ili kuwarahisishia na kuwapunguzia wananchi adha ya kutembea
umbali mrefu kwenda katika ofisi za makao makuu ya mkoa ama wilaya
kufanya huduma za malipo.
Naibu Waziri wa Nishati akiwa ameshikilia utepe kwa ajili ya kuukata
na kuzindua Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu
Mzunguko wa Pili mkoa wa Lindi tarehe 03 Julai, 2021.
Naibu
Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akimkabidhi mama Opeta
Sijui Bure kifaa cha UMETA (Umeme Tayari) kwa ajiri ya matumizi ya
nyumbani kwake Katoka kijiji cha Narungimbe, wilayani Ruangwa, mkoa wa
Lindi alipopokwenda kuzindua Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini
Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili tarehe 03 Julai, 2021
Naibu
Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akizungumza na wananchi
wa kijiji cha Narungombe (hawapo pichani) wilayani Ruangwa, mkoani Lindi
alipokwenda kuzindua Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu
ya Tatu Mzunguko wa Pili tarehe 03 Julai, 2021.
Monday, July 5, 2021
VIJIJI 192 VILIVYOBAKI MKOA WA LINDI KUFIKIWA NA UMEME
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment