Mwandishi wetu Zanzibar
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Daniel Chongolo amesema Watanzania
daima wataendelea kukiamini na kuiunga mkono Chama hicho ambacho ndicho
kimebeba dhamana kulinda amani, umoja, mshikamano na maendeleo
endelevu.
Aidha amesema kwa umuhimu huo kamwe hakipoteza muda wa
kucheza upatu kwa kuwaunga mkono wasiojua misingi ya Nchi yetu na kwa
hilo watasubiri sana, wakati wao wakiendelea na siasa zao za kubomoa
sisi CCM tunaendelea na kasi ya kujenga nchi chini ya uongozi imara wa
Rais Samia na Dkt Mwinyi.
Chongolo amyesema hayo wakati
akizungumza na wanachama, viongzozi na wakereketwa katika viwanja vya
Afisi Kuu ya CCM kisiwandui mara baada ya mapokezi ya sekretarieti ya
Halmashauri kuu ya CCM Taifa.
Amewakumbusha wanasiasa wanaodhani
dola au madaraka inaweza kupatikana kwa shari, vurugu, uvunjifu wa
amani, uvunjifu wa tunu za Taifa, uzandiki, usaliti dhidi ya nchi kuwa
hilo kamwe halitawezekana kwa vile serikali zinazoongozwa na CCM ziko
makini sana.
"Siku za karibuni kumeibuka kikundi cha wanasiasa
kinachotokana na waliokataliwa kwenye sanduku la kura na wananchi, sasa
wanajipitisha pitisha kila pahala wakilalama, wakieneza chuki,
wakiwakebehi viongozi wa nchi, na wakieneza uongo grade A
"Kwa
kujishikiza kwenye masuala wanaliyoyaita ni matakwa ya wananchi kumbe ni
matakwa yao kwani matakwa ya wananchi yalinadiwa na ilani ya uchaguzi
ya CCM ya mwaka 2020/2025, ni vyema wakapumzika maaana hawataambulia
chochote katika madai yao," amesema.
Chongolo alieleza CCM
inaridhishwa sana na namna Rais Samia na Mhe Dkt Mwinyi walivyoanza
hususani katika kulinda amani, usalama, umoja na mshikamano kwani ndio
chachu ya kufanyika kwa maendeleo. Amewataka watanzania waendelee
kuiunga mkono serikali ili nchi yetu ipige hatua kimaendeleo.
Awali
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka amesema
katu CCM hakitatelekeza malengo yake ya kisera ya kutumikia umma au
kupuuzia ukosefu wa huduma za kijamii na kuimarisha uchumi nchini na
baadala yake ikajielekeza katika kubishana na wapigania vyeo na
madaraka bila agenda za ustawi wa wananchi.
Amesema CCM inafahamu
vita ya kupigania uhuru imekwisha na Afrika inajitawala kama ambavyo
muasisi wetu Hayati Baba wa taifa Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Amani
Karume waliwahi kutuasa na kutuusia kuwa vita ya kupigania madaraka,
wakataja vita hiyo itachochewa na mamluki wa kisiasa kupigania madaraka
bila agenda za maendeleo kwa wananchi.
"Niwasihi wanasiasa nchini
wajikite kwenye siasa za maendeleo kwa kutoa fikra na mawazo mbadala
yanayoweza kuchangia kuboresha ustawi wa wananchi na kuharakisha
maendeleo ya nchi yetu. Waachane na siasa za kitoto za kutoa mikwara ya
maigizo kwa Rais Samia, wanaoipinga wafanye ukosoaji unaojenga na sio
unaobomoa na kutishia kutugawa au kuvunja amani ya nchi," Shaka
Ameongeza
katika kipindi kifupi cha utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais
Husein Ali Mwinyi wameakisi mambo yaliyokuwa yakitamaniwa na jamii
yatokee na kufuatwa. Sauti zao zimetoa mwanga zimewapa matumaini mapya
waliokata tamaa na tabasamu akili kutokana na uongozi bora wanaouonesha
unaoheshimu taaluma, kusimamia weledi, utawala wa sheria na kutoa
maamuzi ya haki.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akiwa na viongozi wa Chama hicho wakiwa na aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein ambaye wameenda kumsalimia na kupata baraka zake .
Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(aliyekaa katikati) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Daniel Chongongolo baada ya kufika Afisi Kuu za Chama hicho Kisiwandui Zanzibar
No comments:
Post a Comment