"Huduma za Afya ya kinywa na Meno zinatolewa katika Halmashauri zote 9 za Mkoa, Mkoa una vituo 39 unazotoa huduma hizo, Kama Mkoa unaendelea na juhudi kuhakisha Hospital zote za Halmshauri zinakuwa na Vifaa tiba za kutosha ikiwemo Wataalamu na Upatikanaji wa Huduma ya Dental Exray kwenye Hospital zetu.
Naye Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Dk. Deogratus Kilasara Ameeleza kuwa Mkoa huo umefanya Vizuri katika utoaji wa huduma ya Afya ya Kinywa na Meno kwa kuwa huduma hii inapatikana katika Vituo 39 Kati ya vituo 298 vya Serikali. "Huduma hii inapatika kwa asilimia 13 kulinganisha na huduma zingine za afya na ipo juu kulinganisha na hali ya kitaifa ambayo hadi sasa ni asilimia 7. Ameeleza Mkoa pia unakabiliwa na uhaba wa Wataalam na Vifaa tiba
Naye Mgeni Maalumu kwenye Hafla hiyo Rais Mstaafu awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema " bado kuna mahitaji makubwa ya kuimarisha huduma ya Afya ya kinywa na Meno katika Halmashauri ya Chalinze na Mkoa wa Pwani, ameongeza kuwa bado ipo kazi ya kuendelea kutafuta Vifaa tiba ikiwemo Dental Exray kwa Hospital nane za Halmshauri za Mkoa huo, ambayo kwa Sasa ipo moja tu kwa Mkoa mzima katika Hospital ya Wilaya ya Mafia" Ameeleza kuwa kupatikana kwa vifaa tiba na wataalam ni jambo linalowezekana amewataka kuendelea kujipanga kutatua Changamoto hiyo.
No comments:
Post a Comment