Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imegawa vitabu vya kufundishia mtaala wa Uhasibu katika vyuo mbalimbali vinavyofundisha Taaluma ya Uhasibu nchini. Zoezi hili linahitimisha malengo yaliyowekwa ya NBAA katika wiki ya utumishi wa umma kwa kugawa vitabu Vyuoni na Shuleni. Vitabu hivi vilivyogawiwa ni kuanzia ngazi zote yaani ngazi ya cheti mpaka Shahada ya juu.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno amesema vitabu hivyo vitakuwa na msaada mkubwa sana kwani vitasaidia waalimu wanaofundisha masomo ya Uhasibu pamoja na wanafunzi wanaosoma fani ya Uhasibu kupata vitabu vya rejea.
Pia CPA Maneno amesema kuwa NBAA ina imani wanafunzi watakaomaliza vyuo na kuja kusoma mitihani ya Uhasibu watafaulu masomo yao kwa kiwango cha juu zaidi kwa kuwa wanavitabu vinavyotoa elimu ya uhasibu inayoendana na mitihani ya Bodi hiyo.
Naye Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo, Peter Lyimo ametoa rai kwa waalimu kutumia vitabu hivyo ipasavyo na kuwataka waviweke kwenye Maktaba za vyuo ili wanafunzi waweze kuvipata na kujifunzia na pia NBAA wakija kukagua wavikute vitabu vikiwa vinatumika.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno(katikati) akizungumza na baadhi ya wawakilishi wa vyuo mbalimbali kuhusu ugawaji wa vitabu vya kufundishia mtaala wa Uhasibu katika vyuo mbalimbali vinavyofundisha Taaluma ya Uhasibu nchini katika ofisi za Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo, Peter Lyimo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu na Utawala, Grolia Kaaya.
Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo, Peter Lyimo(kushoto) akizungumza na baadhi ya wawakilishi wa vyuo mbalimbali kuhusu namna walivyojipanga kusimamia utumiaji wa vitabu hivyo pamoja na kufanya ukaguzi wa vyuo hivyo vilivyopewa vitabu ili kuweza kuongeza ufanisi katika matumizi ya vitabu hivyo wakati wa zoezi la kugawa vitabu katika ofisi za Bodi hiyo leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu na Utawala, Grolia Kaaya.
Baadhi ya Wafanyakazi wa NBAA pamoja na baadhi ya wawakilishi wa vyuo mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno wakati wa wakati wa zoezi la kugawa vitabu vya kufundishia mtaala wa Uhasibu katika vyuo mbalimbali vinavyofundisha Taaluma ya Uhasibu nchini.
Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo, Peter Lyimo(kushoto) akigawa vitabu kwa wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya kufundishia mtaala wa Uhasibu hii ikiwa ni kurudisha mchango kwa jamii wakati wa zoezi la kugawa vitabu vya kufundishia mtaala wa Uhasibu katika vyuo mbalimbali vinavyofundisha Taaluma ya Uhasibu nchini..
Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Bodi hiyo na wawakilishi wa vyuo mbalimbali wakati wa zoezi la kugawa vitabu vya kufundishia mtaala wa Uhasibu katika vyuo mbalimbali vinavyofundisha Taaluma ya Uhasibu nchini.
Mhadhili wa Chuo cha CBE, CPA Albinus Majura akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa kuamua kurudisha kwa jamii kwa kugawa vitabu vya kufundishia mtaala wa Uhasibu katika vyuo mbalimbali vinavyofundisha Taaluma ya Uhasibu nchini lililofanyika katika ofisi za Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment