TCRA yawataka wananchi kuhakiki namba zao za simu - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 4, 2021

TCRA yawataka wananchi kuhakiki namba zao za simu

Afisa Tehama wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Upendo Kaluzi akizungumza na wananchi waliotembelea Banda la TCRA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.Wafanyakazi wa TCRA wakiwa katika picha pamoja Mara baada ya kufungua Banda kwa ajili ya kuhudumia wananchi katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Afisa Habari wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Robin Ulikaye akimhudumia mteja wakati alipotembelea banda la TCRA wakati alipotembelea banda la TCRA maonesho 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Semu Mwakyanjala akizungumza na Michuzi TV Kuhusiana taarifa mbalimbali za Mamlaka hiyo katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakioneshwa machapisho yenye taarifa za Mamlaka hiyo.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa Teknolojia ya Mawasiliano inakua kwa kasi kutokana na Teknolojia inabadilika hivyo uhakiki wa namba ni muhimu sana.

Akizungumza katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam Afisa Habari Mwandamizi Mkuu wa TCRA Semu Mwakyanjala amesema wanaotumia huduma za Miamala Kwenye Simu 34 Milioni ambapo ni uchumi mkubwa kwa nchi katika biashara ya huduma za fedha kwa kutumia simu.

Mwakyanjala amesema mpaka Juni 21/2021 Laini za simu za mkononi zaidi Milioni 52 zilizosajiliwa kwa kutumia alama za vidole.

Hata hivyo amewataka wananchi kufatilia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kupata taarifa za mamlaka hiyo.

Aidha amesema jumla ya laini za simu za mkononi zilizohakikiwa ni zaidi Milioni 41 ambazo ni sawa na asilimia 80 ya laini zote zilizosajiliwa kwa alama za vidole.

Amesema idadi ya Laini ambazo bado hazijahakikiwa ni 10,453,447 ambazo ni sawa na asilimi.

Mamlaka hiyo unatoa rai, kwa watumiaji za laini za simu ambao hawajahakiki laini zao kufanya hivyo mapema iwezekanavyo na ifahamike kuwa ni jukumu la kila mtumiaji wa huduma za mawasiliano kuhakiki laini zilizosajiliwa kwa kitambulisho chake.

Aidha amesema kuwa watu wahakiki namba zao pamoja na kutoa taarifa utapeleli katika mamlaka hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad