BENKI ya NMB imekuwa taasisi ya kwanza kutekeleza rasmi mpango wa bima
ya afya kwa wakulima nchini baada ya kuingia makubaliano ya kutoa huduma
hiyo na vyama vikuu viwili vya ushirika mkoani Tabora, ambavyo ni WETCU
na MILAMBO vinavyowakilisha vyama vidogo vya wakulima zaidi ya 200
mkoani humo.
Kupitia mpango wa Ushirika Afya wanachama wa vyama
hivyo wapewa mikopo isiyo na riba na Benki ya NMB kwa ajili ya gharama
za matibabu kwa kutumia kadi za NHIF. Utiaji saini wa makubaliano hayo
na vyama vya wakulima wa zao la tumbaku yanayouhusisha pia Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulifanyika Tabora kama sehemu ya
kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Ushirika.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alizindua rasmi mpango
huo kwa kuwakabidhi kadi za NHIF wakulima wa tumbaku; Kulwa Mfaume,
Saleh Mpemba na Athanas Semeduke ambao ni miongoni mwa kadi 102 za
kwanza ambazo zimetolewa na benki hiyo. Lakini pia kadi 90 zitatolewa
kwa wakulima mkoani Kahama.
Vilevile, aliishukuru NMB kwa mchango wake wa kuviimarisha vyama vya ushirika na kuvifanya kuwa nguzo muhimu ya kiuchumi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi
na Biashara wa NMB, Bw. Filbert Mponzi alisema, NMB imetenga zaidi ya
TZS bilioni 5 kwa ajili ya kuwakopesha wakulima chini ya utaratibu wa
Ushirika Afya. Lakini pia wana mpango wa kuongeza kiasi cha pesa ili
kuwafiki wakulima zaidi ya 300,000 nchi nzima.
Utaratibu huu
utarahisisha kazi ya kuwahamasisha wakulima kijiunga na vyama vya
ushirika na utaongeza idadi ya watu wenye bima za afya kama serikali
inavyotaka na kuelekeza.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB,Filbert Mpozi
(wa pili toka kulia) Mwenyekiti wa WETCU ,Hamza Rajabu wa pili kutoka
kushoto, mwenyekiti chama cha ushirika cha Milambo John Ntezilyo na
kulia kabisa ni Mkurungenzi Mkuu wa mfuko wa Bima ya Taifa ya afya
(NHIF),Benard Konga wakionyesha mkataba wa mikopo wa bima ya afya kwa
wakulima waliosaini na vyama vikuu vya ushirika vya WETCU na MILAMBO
mkoani Tabora.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Kassim Majaliwa (kulia)
akimkabidhi kadi ya bima ya afya mkulima wa tumbaku - Atanas Gabriel
kutoka kikundi cha ushirika Urambo Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Kassim Majaliwa (kulia)
akimkabidhi kadi ya bima ya afya mkulima wa tumbaku - Kulwa Mfaume
kutoka chama kidogo cha ushirika Kabungu Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.
Monday, July 5, 2021
NMB yawa ya kwanza kutekeleza rasmi mpango wa Ushirika Afya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment