Mwenyekiti Umoja wa Vijana Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Taifa, Eng.Aivan Maganza.
MWENYEKITI
Umoja wa Vijana Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Taifa, Eng.Aivan
Maganza azidi kupigilia msumari kuhusu wanaoomba Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya.
Amesema
kuwa kunamakundi 18 yanayoungana katika kutengeneza katiba mpya lakini
ni vyama vya Siasa tuu ndio vinavyopigania kupata katiba mpya na sio
wananchi kama wao wanavyodai.
Akizungumza
leo jijini Mwanza Eng. Maganza amesema kuwa vyama vya siasa ni kundi
moja tuu hivyo halitoshi kuwasemea wananchi kuwa wanataka katiba mpya,
kwasababu kundi moja halishawishi kupata katiba mpya basi wakashawishi
makundi 17 yaliyobaki kwani wao tuu hawatoshi.
Hata
hivyo amzidi kusisitiza kuwa vyama vya upinzani nchini kuacha
kumchonganisha Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi kwa kitendo chao cha
kudai katiba mpya ili hali suala hilo halipo katika ilani ya chama cha
Mapinduzi (CCM).
Hata
hivyo amehoji Chama cha Siasa cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kinachodai Katiba Mpya, Rais atapata wapi fungu la fedha za kuanza
kujadili Katiba? Ingali bajeti ya 2021/ 2021 hakuna fedha zilizotengwa
kwaajili ya katiba mpya.
Hata
hivyo Eng. Maganza amesema kuwa kwa sasa vyama vya siasa viachane na
dhana ya katiba mpya na waache Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
afanye kazi ya kujenga nchi.
Hata
hivyo ameombwa wananchi kujenge nchi kwanza na baadae ikifikia wakati
wa katiba tutaitengeneza katiba mpya na mengine baadae.
No comments:
Post a Comment