HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 9, 2021

NMB ndio Mdhamini Mkuu wa Zanzibar International Marathon 2021

  Benki ya NMB imedhamini mbio za KM 5 za Zanzibar International Marathon 2021 zinazotarajiwa kufanyika 18 Julai mwaka huu zenye lengo la kukuza Utalii na Uchimi wa bluu Zanzibar.

Akizungumza wakati wa uzinduzi mdogo wa utambulisho wa mbio hizo kwa upande wa Tanzania Bara, uliofanyika ndani ya duka la Just Fit Sports Gear Mlimani City, Meneja wa Biashara za NMB Zanzibar, Abdalla Duchi alisema wameunga mkono harakati za Serikali kuiona Zanzibar inakuwa kiuchumi haswa uchumi wa bluu na NMB Zanzibar wameendelea kutoa huduma bora za kibenki ambapo ni moja ya fursa za kukuza uchumi kisiwani hapo.

Aidha, Duchi alibainisha kuwa, NMB imedhamini mbio za KM 5 ambazo tayari viongozi wakuu wa nchi wakiwamo Rais Dkt. Hussein Mwinyi, Makamu wake wa kwanza na wa Pili wa Rais na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wamethibitisha kushiriki. Aliwaasa pia, wananchi kuendelea kujiandikisha kushiriki mbio hizi ili kutangaza utalii na kuimarisha afya zao.

NMB Jogging Club yenye watu zaidi ya 100 kupitia Nahodha wake Jessica Sanga, wamethibotisha kushiriki mbio hizo.

Kwa upande wao kampumi ya Vodacom kupitia kwa Afisa Masoko na Mawasiliano, Kitengo cha Lipa Kwa Simu (Vodacom), Bw. Mario Mpingirwa alisema wametoa punguzo la asimia 10 kwa wateja watakaolipa kwa simu. Washindi katika mbio hizo wataondoka na zawadi nono kama ifuatvyo:

Milioni 3,000,000 kwa washindi wa KM21 kike/kiume, Mil 2,500,000 kwa washindi wa pili na Mil 1,000,000 kwa mshindi wa Tatu huku washindi wengine hadi 10 wataibuka na Tsh Laki moja kila mmoja.

Kwa mbio za KM 10, Mshindi wa kwanza ni Mil 2,500,000, Mshindi wa wa pili 2 ni Mil 1,000,000 na wa Tatu ni Tsh. 750,000. Mbio za KM 5 mshindi wa kwanza ni mil 1,000,000, wa pili Tsh.750,000 na wa Tatu ni Tsh. 500,000.

Aidha, kwa upande wa Walemavu watatoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu pekee ikiwemo Mshindi wa kwanza ni Mil 1,000,000 wa pili Tsh.750,000 na wa tatu ni 500,000.

Unaweza kulipia mtandaoni na pia kwa kujiandikisha kupata fomu za ushiriki kwenye maduka ya Dauda sports, Just Fit sports gear Kijitonyama na Mlimani City na kwa Zanzibar, Cataluna Barbershop iliopo Kiembesamaki, Park Hyatt Zanzibar, Cape Town fish market Zanzibar. 

Meneja Msimamizi wa Biashara za NMB Zanzibar, Abdalla Duchi, akizungumza wakati wa kutambulisha rasmi mbio za Kimataifa - Zanzibar International Marathon katika hafla iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. NMB ni mdhamini Mkuu wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 18, 20021 Kisiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad