Mhasibu na Afisa Utawala wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Usafiri Ardhini (LATRA CCC) Fatuma Kulita akizungumza na wanafunzi waliotembelea Banda la LATRA CCC katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
LATRACCC wakiwa picha ya pamoja na wanafunzi waliotembelea Banda la LATRA CCC katika maonesho ya Sabasaba jijini.
*Ni kuachana na mazoea ya kugombania wakati wa kuingia katika vyombo vya usafiri.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Usafiri Ardhini LATRACCC limesema kuwa wananchi kupanda vyombo usafiri kwa usitarabu kwa kupanga mistari na sio kugombania
Akizungumza na katika Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelalea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Mhasibu na Afisa Utawala wa LATRA CCC, Fatuma Kulita amesema katika kipindi cha hivi karibuni wametoa elimu ya kupanda vyombo vya usafiri kwa Mkoa Dar es Salaam kwa kituo cha Mwendokasi Ubungo na Kimara kuingia katika vyombo hivyo kwa kupanga mstari.
Amesema kuwa elimu inaendelea kutolewa nia ni kutaka kutaka wananchi kujengewa usitarabu ambao kila mtu atapanda chombo cha usafiri bila kukwaluzana.
Kulita amesema kuwa vyombo vya usafiri vinapopata changamoto kwa kwa zile za masafa marefu ndani ya masaa mawili wanatakiwa wawe wamepata suluhisho baada ya hapo wanatakiwa kugharamia kwa Chakula na Kama watalala wanatakiwa kulipia gharama hizo.
Aidha amesema namna ya kutoa malalamiko ni kwenye Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini LATRA na ndipo kuanza kushughulikiwa baraza la Ushauri LATRA CCC.
Amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali pamoja na machapisho juu ya huduma na namna ya kufikisha malalamiko juu ya vyombo vya usafiri ardhini.
Awesome and interesting article. Great things you've always shared with us. Thanks. Just continue composing this type of post.
ReplyDelete