Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti
Naibu
Waziri wa Maji , Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema ,wakazi wa
kijiji cha Mahege na Ruaruke wilayani Kibiti mkoani Pwani ,watarajie
kuondokana na kero ya ukosefu wa maji safi na salama ,ambapo
amewahakikishia kuwa kero hiyo inakwenda kubaki historia.
Aidha
amewatoa hofu wakazi wa Mahege na kusema serikali inatarajia kupeleka
milioni 100 mwezi ujao ,ili kuanza mradi wa ujenzi wa maji kijiji Cha
Mahege,ambao utagharimu milioni 735.761.3 hadi kukamilika kwake.
Aliyasema
hayo ,wakati wa ziara yake ya kikazi , wilayani Kibiti ambapo
ametembelea kijiji Cha Mahege kuzungumza na wananchi na miradi ya maji
Nyamisati, Ruaruke na mradi wa maji wa Miwaga.
Pia
Mahundi ,alimwelekeza mkuu wa wilaya ya Kibiti Ahmed ,kusimamia
kuondosha changamoto ya kuzungusha maji kwa dizeli mradi wa maji Miwaga
,na kumtaka ashughulikie tatizo hilo TANESCO ili uendeshaji ubadilike .
Mahundi
alimtaka meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini
(RUWASA )Kibiti,Pascal Kibanjulo ,kuangalia namna ya kuongeza vituo vya
maji vitano huko Ruaruke ili kusogeza huduma ya upatikanaji wa maji kwa
wakazi .
Alieleza
,serikali inatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kutatua
changamoto ya ukosefu wa maji mijini na vijijini ,hivyo wanaendelea
kupeleka fedha katika miradi mbalimbali ikiwemo miradi viporo iliyofika
hatua nzuri ya ujenzi kwa asilimia 70-90 .
Awali akiuliza
swali, mkazi wa Mahege ,Jafari Ramadhan aliiomba serikali iwasaidie
kutatua changamoto ya maji kwani wanataabika miaka mingi na huduma hiyo
isogezwa maeneo ya shule.
"Imekuwa
kama ahadi hewa ,tunataka kujua mradi unaanza lini na tutapata maji
kuanzia lini ili wake na watoto wetu tupate kunufaika na maji safi kama
ilivyo maeneo mengine"alisema Ramadhan.
Kwa
upande wake ,meneja wa RUWASA Kibiti Kibanjulo alisema ,mradi wa Kijiji
Cha Mahege utaanza agost-septemba na ujenzi wake utachukua miezi sita
hadi mei 2022.
Alieleza
,kwasasa hakuna kupigana kalenda ,watapiga kambi agost mwishoni 2021
hadi ujenzi utakapokamilika na utanufaisha wanafunzi na walimu shule ya
Mahege .
Kibanjulo
alifafanua mradi wa Ruaruke ,ni ukarabati unagharimu milioni 62.406 .8
fedha zilizotumika milioni 45.757.2 utekelezaji umefikia asilimia 75.
Nae mkuu wa wilaya hiyo , Ahmed alisema hali ya upatikanaji wa maji Kibiti ,ni asilimia 69 vijijini na asilimia 65 mjini .
Alibainisha
,katika mwaka wa fedha 2021-2022 kupitia serikali kuu wakala wa maji ,
unaendelea na utekelezaji wa miradi mitatu ya maji Nyamisati milioni
239.264.5,mradi Miwaga milioni 351.726.6 na miradi mitatu ya malipo ya
matokeo (PbR) ambayo ni mradi wa Ruaruke,Uponda na upanuzi wa mradi wa
maji shule ya msingi Jaribu Mpakani.
No comments:
Post a Comment