Na.WAMJW- Dodoma.
Wafamasia nchini wametakiwa kufanya
ajenda ya upatikanaji wa dawa iwe ya kudumu Kwenye kamati za ulinzi na
usalama ngazi ya Kijiji, Kata,Wilaya na Mkoa.
Rai hiyo imetolewa
leo na Dkt.Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto wakati wa mafunzo ya usimamizi na UDHIBITI wa bidhaa za
afya kwa wafamasia wa Mikoa,Halmashauri na Hospitali uliofanyika jijini
Dodoma.
Dkt. Gwajima amesema kuwa ajenda hiyo ikiwa endelevu
Kwenye ngazi hizo Basi hakutakuwa na malalamiko ya upatikanaji wa dawa
yanayoendelea kuwa hauridhishi
"Nitoe maagizo kwa viongozi wa
ngazi zote ,wafamasia wa Mikoa,Halmashauri na Hospitali fanyeni ajenda
ya upatikanaji wa dawa iwe ya kidumu Kwenye kamati za ulinzi na usalama
ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya na Mkoa".Alisisitiza.
Hata hivyo
Dkt.Gwajima aliwataka wafamasia hao kuimarisha kamati za Dawa na Tiba
Katika ngazi zote "Mfamasia ndiye Katibu wa kamati za Dawa na Tiba
lakini kamati hizi hazifanyi kazi zimekufa,naelekeza kuwa wote ambao
kamati zao zilibainika kuwa mfu watoe maelezo kwa mamlaka zao za ajira
na kwa Baraza lao la kitaaluma.
Aidha, Waziri huyo aliwaagiza
wataalamu hao kwenda kusimamia Mwongozo wa Matibabu nchini na Orodha ya
Taifa ya Dawa Muhimu (STG/NEMLIT),kwani mwongozo huo toleo jipya la
mwaka 2021 limezinduliwa.
"Andikeni dawa kwa kuzingatia
mwongozo huu na kuwe na mfumo wa tathmini kwa wale wasiotii kuandika
majina halisi ya dawa (generic names) Bali wanaandika majina ya Biashara
zao(brand names) mkasimamie mwongozo huu"Alisema.
Kwa upande wa
matumizi ya Cheti Cha Dawa Dkt. Gwajima aliwataka wafamasia hao Kwenye
kusimamia Hilo Kama alivyoelekeza awali kanuni ya Cheti Cha dawa 'The
Pharmacy (Prescription Handling and Control Regulations, 2020) kwani
imeandaliwa na imeanza kutumika.
"Sekta ya afya na hasa waandishi
na watoaji wa dawa fuatieni kanuni hii kinyume na hapo utashtakiwa tu
maana haitajulikana Nani alikunywa dawa".
Dkt.Gwajima aliwataka
wafamasia hao kuhakikisha Kuna upatikanaji na matumizi sahihi ya nyezo
muhimu za usimamizi wa bidhaa za afya zikiwemo leja ya Mali na hati
yabkutoa na kupokea Mali,rejista ya dawa,rejista ya sindano na Cheti Cha
dawa.
No comments:
Post a Comment