Kampuni ya mbolea ya Yara yazindua programu ya yaraConnect mkoani Kilimanjaro kutoa elimu ya kilimo chenye tija. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 5, 2021

Kampuni ya mbolea ya Yara yazindua programu ya yaraConnect mkoani Kilimanjaro kutoa elimu ya kilimo chenye tija.

 

 Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw Stephen kagaigai ameisifu kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa mbolea nchini ya Yara Tanzania kwa kuzindua programu ya yaraConnect itakaowezesha wasambaji na wanunuzi wa mbolea hiyo kupata elimu ya utaalamu wa kilimo kwa njia ya mtandao.

Akisoma hotuba hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huyo wa Kilimanjaro, Ofisa kilimo wa Mkoa huo, Simon Msoka alisema kwamba uzinduzi wa App hiyo ni fursa muhimu kwa wakulima kwenye mkoa huo kuweza kupata elimu kuhusu mbolea ya Yara kwa wakati kupitia huduma hiyo mpya ya kidigitali.

Alisema kwamba uzinduzi wa mfumo huo mpya kwenye mkoa wa Kilimanjaro utawezesha wasambazaji na wauzaji wa mbolea za Yara kujisajili na kutoa huduma zao kwa wakulima nchini kupitia simu zao za viganjani.

 “Hii ndio faida ya teknolojia ambayo haikwepeki. Sasa hivi karibu kila nyumba ina simu ya smart na kila mtu anao uwezo wa kuwasiliana kwa njia ya mtandao kwa namna moja au nyingine. Simu imekuwa sio anasa tena bali ni kifaa muhimu cha kazi na elimu pia,’ aliongeza.

Alifafanua kwamba serikali ya Mkoa inashukuru sana kwa kampuni ya Yara Tanzania kuchagua kuja kuanza na mkoa wao na kisha kuelekea katika mikoa mingine.

Afisa kilimo huyo, Bw Msoka aliahidi kwamba serikali itaendelea kushirikiana na kampuni hiyo katika jitihada za kuuletea Mkoa wao maendeleo zaidi kupitia kilimo ambacho ndio moja ya vyanzo vikubwa vya mapato katika mkoa huo na nchi nzima kwa ujumla.

 Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya YarabTanzania, Winstone Odhiambo alisema kwamba kampuni hiyo inayojihusisha na uagizaji na usambazaji wa mbolea hapa nchini kwa miaka 15 hadi sasa ni kampuni tanzu ya Yara International ASA , ambayo inaongoza katika uzalishaji wa mbolea duniani na katika masuala ya utunzaji wa mazingira na lishe.

Aliongeza kwamba moja ya malengo yao ni kubuni mbinu sahihi za kilimo ikiwemo za kidijitali zaidi na kama uzinduzi wa yaraConnect App ambayo inafungua fursa ya kurahisisha biashara kwa kutumia njia ya mtandao.

Alisema kwamba baada ya mkoa wa Kilimanjaro na kampuni hiyo itapeleka huduma hiyo katika mikoa mingine sita ikiwemo Arusha, Tabora, Njombe, Iringa, Mbeya na Morogoro.

“Hii ni App mpya kabisa itakayopatikana kwa kupitia simu za smart na inalenga wauzaji na wasambazaji wa bidhaa za Yara. Leo hii tuko nao baadhi ya wasambazaji na wauzaji ili tuwaelekeze wakawe mabalozi wazuri wa App hii ya YaraConnect nchini,” aliongeza.

Mkurugenzi huyo wa Yara Tanzania, Bw Odhiambo aliongeza kwamba App hiyo ni rahisi sana kupakua kwani watumiaji wa simu za android wataweza kuipakua kupitia Playstore na wale wa simu aina ya iOS wataipakua kupitia Appstore.

Alisema kwamba wasambazaji na wauzaji wa mbolea ya Yara wanaweza kutumia App hii kusajili biashara zao kwa haraka mno, wanaweza kujizolea pointi kwa kupiga picha alama maalumu kutokana na manunuzi ya bidhaa za hadhi ya Premium na wataweza kupata taarifa kuhusu pointi zao na kutumia pointi hizo wanapotaka kujizolea zawadi zao mbali mbali kama Pikipiki, simu, pesa taslimu na zawadi nyinginezo.

Alitoa rai kwa wasambazaji wote wa bidhaa zao wachangamkie fursa hiyo na kuna ahidi kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro katika kuendelea kubuni mbinu nyingine za kidijitali zaidi ili kuhakikisha wadau wa kilimo nchini wanapata mafanikio.

Yara ni kampuni ya Mbolea iliyojidhatiti kuwekeza na kuendeleza kilimo hapa nchini na uzoefu ka takribani miaka 15.

Ofisa Kilimo Mkoa wa Kilimanjaro na mwakilishi wa mkuu wa mkoa huo, Simon Msoka akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya yaraConnect yenye lengo la kutoa elimu ya utaalamu wa kilimo kwa njia ya kidigitali. Hafla hiyo ilifanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro leo. Kushoto kwake waliokaa ni, Mkurugenzi Mtendaji wa Yara Tanzania, Winstone Odhiambo na Bwanashamba Mkuu Mwandamizi wa Yara, Maulidi Mkima.
.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhambo akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya yaraConnect yenye lengo la kutoa elimu ya utaalamu wa kilimo kwa njia ya kidigitali katika hafla iliyofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro leo

Bwanashamba Mwandamizi wa Kampuni ya mbolea ya Yara, Maulidi Mkima, Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya yaraConnect yenye lengo la kutoa elimu ya utaalamu wa kilimo kwa njia ya kidigitali. Hafla hiyo ilifanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro leo. Kushoto kwake waliokaa ni, Mkurugenzi Mtendaji wa Yara Tanzania, Winstone Odhiambo na Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Msoka aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo katika uzinduzi huo

Baadhi ya mawakala na wadau wa mbolea ya yara wakipiga picha na viongozi wa yara na kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro muda mfupi baada ya uzinduzi huo. 

Mmoja wa mawakala wa mbolea ya yara akisoma kipeperushi kupata taarifa mbalimbali za faida ya kujiunga na programu ya yaraConnect katika uzinduzi huo mjini Moshi, Kilimanjaro leo.

Baadhi ya mawakala na wauzaji wa mbolea ya Yara wakihudhuria uzinduzi wa yaraConnect App mjini Moshi, Kilimanjaro leo. 

Meneja Masoko wa Yara, Sheila Chatto (wa pili kulia), akitoa maelekezo ya jinsi ya kujiunga na yaraConnect App kupitia simu ya mkononi kwa baadhi ya wateja wao waliohudhuria uzinduzi huo mjini Moshi, Kilimanjaro leo. 

Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Yara, Deodath Mtei (kulia) akizungumza jinsi programu ya yaraConnect App inavyofanya kazi na faida zake.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhambo (kushoto), akiagana na Ofisa Kilimo Mkoa wa Kilimanjaro na mwakilishi wa mkuu wa mkoa katika hafla hiyo, Simon Msoka mara baada ya uzinduzi rasmi wa yaraConnect App mjini Moshi, Kilimanjaro leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad