Kampuni ya Gf Trucks & Equipment’s Ltd ya jijini Dar es Salam imewaomba Watanzania hasa wadau wa sekta ya ujenzi na usafirishaji kupenda kununua bidhaa za ndani ili kusaidia kukuza uchumi.
Akizungumza katika banda la Kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Sabasaba, Afisa Masoko wa GF Truck Juma Lukolo amesema, kama Watanzania watajenga utaratibu wa kununua bidhaa za ndani basi pia wataokoa fedha nyingi za kigeni.
Amesema Watanzania wamekuwa wakitumia fedha nyingi za kigeni na tena kwa gharama kubwa kuagiza magari kutoka nje, hivyo kwa magari haya kutengenezwa humuhumu nchi kutaokoa muda, gharama na kusaidia kukuza uchumi wa ndani.
"Kwa sasa yale magari tuliyokuwa tukiagiza na kuyauza kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo sasa tunayatengeneza hapahapa nchini kwa lengo la kukuza uchumi, kutoa ajira kwa Watanzania huku tukikuza uchumi.
Kiwanda kinachotengeneza magari hayo cha GF Truck and Car Assemble ambacho kipo ndani ya majengo ya iliyokuwa Tamco.
No comments:
Post a Comment