MKUU wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro leo Ijumaa 02/06/2021 amefanya Kikao na Watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Lushoto na kujionea Upatikanaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa Hospitalini hapo pamoja na Kutembelea na kukagua jengo jipya la Hospitali ya Wilaya ya Lushoto.
Pia amemuelekeza Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ndugu Gastro S Laswai Kuboresha upatikanaji wa Huduma za Afya mfano Kitengo cha Mortuary kwa kuhakikisha Majokofu yote sita (6) yaliyopo Hospitalini hapo yanafanya kazi vizuri, Kudhibiti Upotevu wa dawa na Kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato na Kuhakikisha dawa na huduma nyingine muhimu zinapatikana kwa wakati kwa Wanachi huku akiagiza mtambo wa Ultrasound uliokuwa umeharibika kifaa cha "Adaptor" uanze kufanya kazi mara moja, Kuboresha huduma za Mama na Mtoto, Kuboresha na Kuweka Miundombinu rafiki kwenye Madirisha ya kutolea Huduma kwa Wazee.
No comments:
Post a Comment